Watoto wa Marehemu Gurumo wagombania mali za baba yao

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
"Tunatoana roho yarabiii, kwa mali alizoacha baba…
" hicho ni kibwagizo katika wimbo wa Tunatoana Roho uliopigwa na Msondo Music Band ‘Sikinde'ukiwa ni utunzi wa marehemu TX Moshi William akishirikiana na marehemu Muhidin ‘Maalim' Gurumo na waimbaji wengine wa bendi hiyo!

Yawezekana Gurumo alikuwa akijitabiria kitakachotokea baada ya kifo chake kwani kabla hata arobaini ya kifo chake ikiwa bado haijatimia, songombingo la aina yake limezuka katika familia yake baada ya watoto kudaiwa kuanza kuzigombea mali alizoziacha baba yao.



GARI ALILOPEWA NA DIAMOND
Utata umeanzia katika gari aina ya Toyota FunCargo alilopewa zawadi na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz' ambapo inadaiwa kuwa mtoto mmoja wa marehemu (jina tunalo), ameshajitangazia kuwa ni lake.



Msanii wa bongo freva Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz' akimkabidhi funguo ya gari aina ya Toyota FunCargo mzee Gurumo
Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho ni ndugu wa karibu wa familia hiyo, siku moja baada ya msiba, mtoto huyo alitangaza kuwa gari hilo ni lake na akaanza kutafuta madalali wa kuliuza gari hilo lakini akakwamishwa na kukosekana kwa kadi ya gari.

"Yaani hawa watoto wa marehemu sijui wana nini jamani, hata arobaini ya baba yao bado wameanza kushikana mashati, hii ni hatari sana. Huyo mmoja ndiyo anajitapa kabisa kuwa gari ni la kwake na ameshaanza kutafuta mteja," kilisema chanzo chetu kwa masharti ya kutotajwa gazetini.

DALALI WA NYUMBA ANATAFUTWA


Yote tisa, kumi ni nyumba aliyokuwa anaishi marehemu na familia yake, iliyopo Makuburi, Ubungo. Kwa mujibu wa chanzo chetu, nyumba hiyo tayari ipo sokoni na madalali wanahaha huku na kule kusaka wateja ili iuzwe.

"Mjane wa marehemu anatia sana huruma. Unajua bado yupo kwenye eda, hata arobaini ya mumewe haijafika watoto wameanza kumchachamalia wanataka kuuza hata nyumba anayoishi, sasa ataenda wapi?
Tunaomba nyie waandishi wa habari mumsaidie huyu mama, watamdhulumu kila kitu," kilisema chanzo.


Mke wa marehemu mzee Gurumo Pili Nassoro

UWAZI KAZINI

Baada ya kupata taarifa hizo, Uwazi liliamua kuingia mzigoni ili kuupata ukweli wa madai hayo mazito.

MSIKIE MTOTO WA MAREHEMU

Uwazi lilimtafuta mtoto wa marehemu, Mariam Gurumo ambaye alipoulizwa kuhusu ishu hiyo, alisema:

"Aliyekupa hizo taarifa ni muongo, hakuna ishu kama hiyo. Kwanza bado tunaomboleza kifo cha baba yetu. Sasa tuuze gari na nyumba ili iweje? Siyo kweli.

"Ni kweli kuna kesi ya nyumba ipo mahakamani lakini siyo nyumba hiyo unayoisema. Unajua sisi watoto wa Gurumo tunataka kudhulumiwa nyumba iliyoachwa na marehemu mama yetu iliyopo Ilala.

"Unajua huyu mjane wa marehemu, hakubahatika kupata mtoto, sisi mama yetu ni marehemu na tulizaliwa wanne, mimi (Mariam), Mwalimu, Mwazani na Omary.

"Abdallah yeye ana mama mwingine lakini ni ndugu yetu wa damu. Kabla mama hajafa, Gurumo alimjengea nyumba Ilala.

"Sasa mama yetu alipokufa, mdogo wake (jina tunalihifadhi) akawa anataka kuiuza, hivi jana tu (Ijumaa) tumetoka mahakamani. Tumefungua kesi pale yenye jalada namba RB/IL/112/2013 kuzuia nyumba kuuzwa. Tunashukuru mahakama imeingilia kati vinginevyo tungedhulumiwa.

Naomba watu wasichanganye, nyumba yenye matatizo ni ya Ilala. Kuhusu gari, kwa sasa bado hatujaamua chochote mpaka arobaini ipite," alisema Mariam.

HUYU HAPA MJANE WA MAREHEMU


Uwazi halikuishia hapo, lilienda mpaka nyumbani kwa marehemu nakuzungumza na mjane wa marehemu, Pili Nassoro ambaye alifunguka mazito. Hebu msikie:


Binti wa marehemu mzee Gurumo Mariam Gurumo

"Ni kweli nyumba inauzwa. Hilo lilikuwa ni agizo la mume wangu kabla hajafariki, aliniambia ni bora aiuze kabla hajafa kwani anawajua wanaye watanisumbua sana pindi akifa.

"Tulianza kutafuta wateja miezi minne kabla Gurumo hajafa, bahati mbaya ametangulia kabla hatujakamilisha hiyo kazi. Yeye alikuwa na lengo zuri la kutaka atugawie kila mmoja chake ili akifa yasitokee haya yanayotaka kutokea.

"Unajua hii nyumba tumejenga na mume wangu, mimi nilikuwa mfanyabiashara na tulisaidiana kabla hata hawa watoto hawajazaliwa lakini nashangaa wanataka kunigeuka eti mimi sihusiki."

MJANE AILILIA SERIKALI IMSAIDIE


"Naomba serikali iingilie kati kwenye hili suala, nyumba wala gari viziuzwe kwanza. Jamani hata eda sijamaliza mambo yameanza kuwa hivi.
Hao watoto wenyewe tangu tumzike baba yao hawajakanyaga hata hapa nyumbani kunijulia hali, sijui wanafikiria nini kuhusu mimi, naomba mnisaidie nimalize eda salama na mali zikiuzwa, basi na mimi nipewe staahili yangu," alisema mjane huyo kwa huzuni.
 
Mara nyingi kuzaliwa matumbo tofauti,Ni mtihani tosha kwenye mali.
 
Ndo shida hiyo watoto wanje mzazi akitoka tu wanawaza mali badala kumtunza mjane
 
Tatizo ni hao waliotuletea habari ni wepesi kuchanganya habari ili wauze hata ukisoma utaona kuna utata hapa.
 
Well said mkuu, tatizo hatuna utamaduni huo, unaandika halafu unauhifadhi wapi kama huna wakili binafsi

Unaweza kuhifadhi mahakamani maana kuna watu wanahifadhi hati za nyumba mahakamani kuogopa kuchezeana shere ndani ya familia.
 
Nilisema kile kigari alichopewa na domo kitaleta shida sana
 
Hawa watoto hawana akili hata kidogo.Wanachojua wao ni uroho wa mali na sio utu.Jaman tunakwenda wapi ebu tumuogope mungu atakuja kutuchoma cku hiyo ikifika.Watoto wana roho mbaya hawamuonei huruma mama yao na wamesahau km kuna mungu anawaona.Naomba serikal imsaidie huyu mama.
 
ila baba yao aliimba ule wimbo sasa wameshindwa hata kuusikiliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…