Watoto wa Mengi wamburuza mahakamani Jacqueline Mengi "Klynn"

So sad mali atafute mwingine kugombania wengine
Life hili daah
 
Hapo ndipo ninapoikubali sheria yadini yakiislam haruhusu kuacha usia wa mirathi kwa wale watakaokurithi yaani watoto wako au wazazi au mke.ila unaweza kuusia wale wasio kuwa warithi wako wapewe kiasi ktk mali yako naimewekwa kiasi kabisa isivuke hapo.rafiki yako kaka dada au hata ndugu yeyote unaweza kuusia apewe ila ktk kiasi kilichotajwa kisivuke hapo
 

Ni kweli K.Lyn ana wakati mgumu kuthibitisha uhalali WA wosia huo Mahakamani.

Lakini MTU anaweza akamwachia urithi wake wote wa Mali KWA MTU yeyote yule anayempenda, hata kama siyo ndugu yake, mwenye mali ana haki ya kufanya hivyo. K.Lyn kilichomgharimu hapo ni kutokana na "shule ndogo kichwani", NA ushauri mbovu alioupata kutoka KWA washauri wake.

Kabla Mzee Mengi hajafariki dunia, yeye K.Lyn angemshawishi mzee ili aandike wosia ambao ni lazima " ungeshuhudiwa NA Mahakama ", NA wala siyo Wakili au kamishina WA viapo WA kawaida kama ilivyofanyika. Angemshawishi KWA nguvu zote ili akubali kuacha wosia ambao ni lazima " Ushuhudiwe NA Mahakama", tena angechagua Mahakama ya juu, kama vile Mahakama ya Wlaya, mkoa, au Mahakama KUU, NA sana sana ingekuwa Mahakama KUU ndio ingependeza zaidi.

Endapo kama Mzee Mengi angeacha wosia ambao umeshuhudiwa NA Mahakama, vurugu zote hizi zisingetokea hata kidogo.

Kuna watu ambao Mimi binafsi nawafahamu vizuri kabisa waliwahi kukumbana NA mkasa na kesi kama hii.Baba yao mzazi aliacha wosia NA kuwanyima Mali zake zote kabisa watoto wake wa kuwazaa wapatao watano, badala yake alimkabidhi urithi wake wote KWA mjukuu wake mmoja tu ambaye alikuwa anamjali. Mzee huyo alipofariki dunia, ulizuka ugomvi mkubwa sana sana WA kugombea urithi kati ya watoto wa marehemu NA mjukuu wake aliyeachiwa urithi.Kesi ilikuwa nzito ilienda mpaka Mahakama KUU, kwa kukatiwa rufaa. Mwisho WA siku mwaka 2007 mjukuu alishinda Kesi hiyo, NA hatimaye Mali zote za urithi zilirejeshwa na kukabidhiwa KWA mjukuu aliyeachiwa urithi.

Nakumbuka watoto wa mmarehemu walinyang'anywa kila kitu, mashamba, nyumba tatu, magari, etc.Tena waliondolewa kwenye nyumba za urithi za marehemu baba yao mzazi kWA nguvu NA Jeshi LA Polisi baada ya mjukuu kushinda rufaa yake ya Kesi Mahakama KUU.

Kitu kilichomuokoa mjukuu kushinda Kesi ni kwamba wosia WA mgawo WA mali za urithi/mirathi uliidhinishwa NA Mahakama, Mzee mwenyewe binafsi kabla hajafa alienda kuandika wosia Mahakamani, na kisha Mahakama iliidhinisha Wosia huo, Baba yao aliamua kuwafunza adabu watoto KWA sababu watoto wake walikuwa NA viburi , walikuwa wanamdharau Mzee wao. Ktk kuwakomesha watoto wake wenye viburi, baba yao mzazi aliamua kuwanyima mirathi, wote waliambulia patupu. Mjukuu alikabidhiwa Mali zote za marehemu.
 
Klyn ashukuru amepata nyumba ya Dar na Machame, watoto watasomeshwa tu.
Angekuwa na akili angetulia tu,mtu kaja jana na hata hajui kampuni zinaendeshwaje au zilianzishwa vipi anataka leo hii apore kila kitu,kweli mal... hawana akili,lakini pia hili ni anagalizo kwa akina mugabe wanaoa wajukuu zao,haya ndio aliyoyata Mzee Machache,alinogewa na aslai hadi akachonga mzinga.Huyu dada alijipanga kete toka mwanzo,kila mwanaume anayekuwa nae anamliza,kuanzie Kinje, Mafia mbulgaria mchezesha kamari na msururu ni mrefu kama mto Rufiji
 
Ila huyo mzee alikuwa ndina kweli kweli tofauti kabisa alivyo kuwa akijinadi kwenye kadamnasi
Ndugu yangu ni wanaume wachache wana jeuri mbele ya nyumba ndogo hasa ikiwa ni wale waliokubuhu,si ajabu mzee alikuwa anaadika hiyo mirathi huku anafanyiwa massages,hapo lazima akili iruke.Au umeshasahau zile clip za video za mwishoni alipokuwa anaimbiwa mapambio ya baby ,baby.
 
Mshenzi yule alinajisi watoto wa watu. Mshenzi mwezie kamtoa. Kuonyesha ushenzi wake kaoa mfanyakazi wa ngazi ya juu wa serikali! Kuna wezi wa kuku jela hawapati msamaha...
Mkuu tulisema hapa kuwa jamaa ni kweli kawaharibu wale watoto.mijitu mizima kwa kulewa minyimbo ya kizamani ikawa inamtetea,wakati watoto walipimwa na wakasema hadi mnara wake ulivyo,na hata alipojitetea kuwa mnara hausomi signal,watu wakasema huo ni uongo na Mungu katuonyesha, kwa kuoa.Na sijui kwanini hajarudishwa kwao.
 
Iv jack hana aibu mzee alikuwa tajiri kitambo yy kaja jana anataka vyote km aliyetafuta hayupo yeye hofu imepotea kabisa
 
Reactions: amu
Wanatoana roho yarabii ii,kwa mali aliziacha baba,bora nikae pembenii, niinusuru mama roho yangu mimi..!!
 
Yani Regina alivyokuwa anamjali baba na alivyokuwa anaijali EA media leo eti ili apate walau buku inabidi hadi ashinde kesi duuuh! Hapa naunga mkono mtu aangushwe tena haraka sana!
 
Kwa hiyo unadhani hawajaliona hilo?Wabongo wajuaji sana,wao ndio wanajua baba yao alikua anaumwa nini na watakua wameshapewa ushauri na Wanasheria na Ma Dr
 
Kesi yako ni irrelevant na ya Mengi,kasome sheria ni vitu gani vinaweza kufanya mzazi aondoe watoto kwenye wosia,hao wa kwako walifanya moja ya vitu ambavyo kisheria vinaweza kuwanyima urithi
 
Hiyo ni sheria.Kwani wewe huna uwezo wa kumpa mtu mwingine mali yako pasipo maoni ya watoto wako?
Hakuna sheria ya hivyo,Mahakama inaupiga chini,unless nithibitishe walitaka kuniua au wa kiume alizini na mke wangu au hawakuwepo kwenye maisha yangu au kama ni sheria ya Uislamu mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa (ingawa nayo,Mahakama ikiona nilimuhalalisha inampa urithi)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…