kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,677
Mwaka 1953 mchumi mashuhuri duniani, Ragnar Nurkse alitoa tafsiri ya umaskini akisema kuwa ni sawa na duara na kwamba mtu akizaliwa maskini ni rahisi kufa maskni kama hakupata nguvu ya ziada ya kumuondoa kwenye hali hiyo.
Katika nadharia yake ya vicious circle of poverty anasema umaskini unatokana na mtu kuwa na kipato kidogo, kama mtu ana kipato kidogo sana, hawezi kuwa na akiba, asipoweza kuwa na akiba haweza kufanya uwekezaji wowote kwa kuwa hana mtaji na kama hakuna uwekezaji huwezi kuendelea na hivyo atabaki kuwa maskini.
Duara hilo la umaskini linaonekana hata kwenye elimu, hasa kwa nchi kama Tanzania, mtoto akizaliwa na wazazi walioenda shule kuna uwezekano mkubwa ya kupata frusa ya kwenda shule na kama wazazi wake hawakupata fursa hiyo ni vigumu mtoto wao kusoma.
Hiyo ndiyo picha halisi ya maisha ya watoto wanaotoka katika familia masikini zenye malezi hafifu, hivyo kuwafanya watoto wazurure mitaani kujitafutia maisha.
Nimezungumza na watoto kadhaa wanaoishi mitaani katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam ili kujua maisha yao halisi na hatima yao ya elimu.
Hakuna wa kutuma elimu
Juma Hussein (16) ambaye makazi yake ni stendi ya mabasi yaendayo mikoani ya Ubungo anasema kuwa alizaliwa Unguja Zanzibar na alikuja bara baada ya baba yake kufariki na hivyo mama yake kuamua kurudi nyumbani kwao mkoani Arusha.
Baba alivyofariki tulirudi nyumbani kwa bibi, tulivyofika Arusha, mimi nilikuwa nasoma Shule ya Msingi Imbaseni, nilisoma mpaka darasa la tano nikaacha Shule.
Anasema kuwa, sababu iliyomfanya aache shule ni hali ngumu ya maisha kwani ilifika mahali hata sare za shule alikuwa hana na chakula nyumbani kilikuwa cha shida sana.
Maisha nyumbani yalikuwa magumu mpaka ikafika mahali nikahama nikawa naishi mtaani ingawa bado nilikuwa naenda shule, nilipoona maisha yamekuwa magumu zaidi nikahamia Arusha mjini, anasema Hussein.
Anaeleza kuwa, baada ya kuona maisha ya Arusha ni magumu yeye na watoto wengine wawili waliamua kuja Dar es Salaam kwa matumaini ya kupata unafuu wa maisha.
Wenzangu wameshakufa, mmoja aliitiwa mwizi akapigwa akafa na mwingine aliumwa tu akafa, mimi bado nipo lakini maisha ni magumu sana, anasema:
Hapa mjini maisha bila kusoma ni magumu sana asikwambie mtu kaka, najua sana kwa kuacha shule lakini sikuwa na namna kwa sababu kwenda shule nikiwa sina nguo na bila kula isingiwezekana.
Anasema kuwa, kwa sasa hajui nini hatima ya maisha yake kwa sababu kila kukicha maisha yanazidi kuwa magumu na hajui ni kwa mfumo gani anaweza kupata elimu.
Hussein anasema kuwa angepata elimu ingeweza kumtoa kwenye maisha magumu aliyonayo.
Kwa haya maisha ya kuokota chupa za majini na kuomba pesa kwa wapita njia siwezi kwenda shule, Mungu tu ndiyo ataamua sasa hatima yangu huko mbele, anasema.
Naye Josephat Alan (14) ambaye analala eneo la feri, anasema alianza kuishi mitaani toka akiwa na miaka 10.
Mtoto mtoto huyu ambaye ni mzaliwa wa Tabora anasema alikuwa akiishi na shangazi yake baada ya baba na mama yake kufariki.
Anasema kuwa shangazi yake huyo hakutaka kumpeleka shule hivyo ilikuwa ni rahisi kushawishiwa na rafiki yake kuja Dar es Salaam.
Huyo rafiki yangu aliniambia ananileta Dar es Salaam kwa dada yake niwe ninamsaidia kazi na kuwa atanipeleka shule, anasema na kuongeza:
Tulivyofika Ubungo, aliniambia hana dada anayehishi huku na kwamba maisha yake ni ya mitaani. Aliniambia kuna Mwarabu ananunua watoto na kuwafanya wanawake (mashoga), kwa hiyo akaniambia anataka anipeleke huko, ikakataa na nikasema nitaishi ninavyojua, anasema.
Anasema kuwa, alivyona hali imekuwa hivyo matumaini ya shule yaliyeyuka na akaanza kuona uchungu wa maisha.
Anaeleza kwamba, mara kadhaa watu wanaodai kutaka kuwasaidia watoto wa mitaani walifika katika eneo analolala ili kuwandisha majina na baadaye wapate msaada wa elimu lakini hajawahi kuona wakirudi.
Maisha bila elimu bora ufe tu, hapa kuna siku unakuwa unaumwa huwezi kwenda kutafuta hata hizo chupa ili uuze na hakuna mtu wa kukusaidia, unalala tu ndani unasubiri wenzako wakaokote hata chakula huko waje wakupe, anasema:
Wakija hao waliosoma wanatuandika majina na kutupiga picha wanasema watakuja kutuchukua watupeleke shule lakini hakuna kitu, tunabaki tukiteseka tu hapa.
Samuel Justine (12) anasema kuwa, yeye amezaliwa na kujikuta akiishi mitaani na kuwa hajui maisha mengine zaidi ya hayo.
Anasema kuwa, hamjui baba yake na mama yake huwa anamueleza kuwa tangu akutane naye na kumpa mimba hajawahi kumuona tena.
Mtoto huyo anasema kuwa yeye pamoja na wadogo zake watatu wanaishi kwa kutegemea kupewa fedha na wasamaria wema.
Tunaomba tutakachopata tunakula pamoja na mama yetu, kwa sasa mama huwa haji na sisi mara nyingi, wanasema.
Anasema kuwa, huwa anaumia sana akiona watoto wa rika lake wakienda shule lakini hana jinsi kwa kuwa mama yake hana uwezo wa kumpeleka shule na kutafuta fedha ili wale.
Anasema kuwa, haoni kama kuna dalili yoyote ya kwenda shule na kuwa maisha anayoishi kwa sasa anadhani ndiyo ambayo Mungu amependa ayaishi.
Mbali na watoto hao kukosa fursa ya kwenda shule, wengi wao wanaishi maisha hatarishi ya kutumia dawa za kulevya na kulawitiwa huku wale wa kike wakibakwa na wakiume kulazimishwa kulawitiwa.
Kubakwa na kupata ukimwi
Maeneo ya feri nilionana na msichana alisema kuwa ana miaka 14, ambaye alianza kuishi mitaani akiwa na miaka 10 baada ya wazazi wake kufariki na yey kutekelezwa na ndugu zake.
Anasema kuwa, baada ya kuona maisha nyumbani yamekuwa magumu alitoroka na kuanza kuishi mitaani.
Zamani tulikuwa tunasimama pale fire tunaomba na watu wanatupa hela maisha yakawa yanaenda, anasema.
Anaeleza kuwa, mara kadhaa kuna watu walikuwa wanaenda katika eneo la mnazi mmoja ambapo wanalikuwa wanalala na kuwaingilia kwa nguvu.
Anasema kwamba, kwa mara ya kwanza mtu aliyemlazimisha kumuingia alikuwa anamlinda na hakutaka mtu mwingine alale naye.
Kwake anasema hiyo ilikuwa afadhali kwani wenzake kila siku walikuwa wakilazimishwa kulala wa watu tofauti tofauti.
Anasema kuwa, baadhi ya watu hao ni vijana wenye umri mkubwa ambao nao huomba, watu wazima ambao huomba pamoja na wapiga debe kwenye vituo vya daladala.
Niliishi hivyo mpaka nikazoea nikawa naona ni kawaida tu, siku moja kuna watu walikuja pale mnazi mmoja wakawa wanapima ukimwi na mimi nikaenda nilivyopima wakaniambia nina ukimwi, anasema.
Mtoto huyo ambaye kwa sasa afya yake imedhoofika sana, anasema kuwa hajui ni nani aliyemuambukiza ugonjwa huo kwa sababu wengi waliokuwa wanamuingilia walikuwa hawatumii kondom.
Mtoto huyo anasema kuwa, kwa nyakati tofauti alijifungua watoto wawili lakini wote walifariki dunia wakiwa wachanga.
Watoto wa kiume kulawitiwa
Mwananchi pia iliwahi kufanya uchunguzi juu ya maisha ya vijana hao na kubaini kuwa, wengi hulazimishwa kulawitiwa ama kulawiti.
Wanakuja usiku kwenye maeneo tunayolala wanatafuta wanayemtaka ili akawafanye, ukimaliza wanakupa hela na wengine wanakunyima wanakufukuza, anasema mmoja wa watoto hao.
Watoto hawa, licha ya matatizo wanayokutana nayo, wakati mwingine huonekana kama wasiostahili kuonekana machoni mwa baadhi ya watu, haswa viongozi wa kitaifa.
Mtoto mwingine akieleza huku akibubujikwa na machozi anasema kuwa, siku ya nne taku akifike Dar es Salaam akitokea nyumbani kwao Dodoma alikuwa amelala kwenye kibaraza cha jengo la Soko la Kariakoo, alianza kusikia maumivu makali sana sehemu za haja kubwa, aliposhituka alijikuta katika mikono na mwaume aliyemwita mzee ambaye alikuwa akimlawiti.
Nilitaka kupiga kelele lakini alikuwa amenibana mdomo na amenielekeza sehemu ya ukutani, alikuwa amechukua maboksi mengi akawa ameyaweka yametufunika kabisa, haikuwa rahisi kwa mtu kuona kilichokuwa kikifanyika, kwa hiyo nikashindwa kumfanya chochote, alipomaliza akaniambia nikipiga kelele ataniuwa, anaeleza na Kuongeza:
Baada ya kunifanya vile sikuweza kulala tena siku ile, kama baada ya wiki kupita, yule mzee alikuja tena na kunikamata kwa nguvu na kuniingiliia tena nikiwa tena nimelala, sasa ikawa ndiyo tabia yake mpaka ikabidi mimi nihame lile eneo nikaja huku Uhindini.
Mbali na mzee huyo anasema pia kwa nyakati tofauti amewahi kukamatwa na vijana wa wanaoishi mitaani ambao ni wakubwa na wakamlawiti.
Watoto wengine wanasema kwamba, baadhi ya watu hufika kwenye maeneo wanapoishi na kusema wanataka kuwapeleka shule, kinyume na wanavyosema huwachukua na kwenda kuwalazimisha kufanya ngono kinyume na maumbe..
Source: MCL