Je, serikali imeshindwa kabisa kuwaondoa na kuwadhibiti watoto hawa wa mitaani wanaolala chini ya daraja la Ubungo(Kijazi interchange) na ambao wamekuwa wakifanya kazi ya kusafisha vioo vya magari?
Sasa hivi wamejijengea tabia ya ajabu kabisa ya kutaka kusafisha kwa nguvu vioo vya magari, sasa ukiwazua, subiri taa zikiruhusu ndio utaelewa. Wamekuwa wakigonga vioo na kumwagia maji yao machafu ndani ya gari
Juzi kati walipishana na dereva wa daladala katika hatua hiyo hiyo ya kulazimisha vitu, Taa iliporuhusu walikuwa wameshajikusanya walivamia daladala na kuanza kuligonga huku wakimwaga maji yao yale ya kuoshea ndani ya daladala.
Nimeshuhudia tena katika gari binafsi, ameanza kusafisha kioo dereva akamzuia, Gari zinaruhusiwa tu, walianza kulipiga gari na kugonga vioo na walijikusanya sijui hata walipotokea.
Sasa hali hii imekuwa kero ukifika ubungo mataa muda wote unakaa kwa wasiwasi. Tabia hii ikikomaa itakuwa hatari zaidi wadhibitiwe mapema