Watoto wa mke mkubwa tukutane hapa

Labda kwa nyie wanawake kwa wanaume tunapotezea na tusingeweza shuhudia hayo yakifanyika mbele ya macho yetu
Sijua kwa miaka yenu, i'm above 40s kwahio kaka zangu ni watu wazima sana, lakini i can tell wako na psychological problems.

na pia hapa naongelea maisha ya vijijini, umetoka shule unaenda kusaidia kuchuma majani ya ng'ombe, wengine kuchota maji mtoni wengine kupika, ile mnaanza kula baada ya kazi za kutwa na njaa imebana hasa, tonge la kwanza la ugali unachovya kwenye maharage...kutia mdomoni unakutana na bonge la chumvi. Yani ni kama mfuko wa chumvi umetiwa kwenye chakula maksudi na alietia hiyo chumvi wote mnamjua......sidhani kama hawa wanaume (kaka zangu) wamepotezea akilini mwao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…