kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 277
SUALA la uchakachuaji mitihani limeingia katika sura mpya baada ya kuibuka kampuni zinazoendesha biashara ya kuwaandikia ripoti za utafiti, wanafunzi wanaohitimu elimu ya juu katika vyuo vikuu.
Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa kampuni hizo hutengeneza kazi hizo, ambazo baadaye huziandika ili zionekane zimefanywa na mwanafunzi husika baada ya kukamilisha malipo.
Wanafunzi hao ni wale wanaomaliza elimu ya juu katika vyuo vikuu mbalimbali nchini katika ngazi ya shahada, shahada ya uzamili na shahada ya uzamivu (PhD).
Wanafunzi wengi kabla ya kukamilisha mafunzo katika ngazi husika kwa kawaida hutakiwa kufanya utafiti na baadaye kuandika ripoti kuhusu taaluma aliyosomea, lakini kwa kuona ugumu wa kazi hiyo, wenye uwezo hutumia kampuni hizo ili kufanyiwa kazi hiyo tena kwa ustadi wa hali ya juu.
Uchunguzi unaonyesha kuwa wanafunzi wenye tabia hiyo wengi wao ni watoto wa vigogo ambao hutumia ipasavyo uwezo wa kifedha wa wazazi au baadhi ya wale wanaosoma huku wakiwa kazini.
Wanafunzi hao inaelezwa hutoa kati ya Sh2 milioni hadi saba ili kupata taarifa za tafiti wanazozihitaji zikiwa tayari zimetengenezwa katika mfumo wa kitabu.
Baadhi ya wahadhiri wa vyuo vikuu mbalimbali nchini wamekiri kuwapo kwa vitendo hivyo wakieleza kuwa walivibaini baada ya kuwauliza maswali wanafunzi kuhusu tafiti walizoziwasilisha, lakini wakashindwa kujitetea.
"Mmoja aliandika tafiti nzuri. Nikawa na wasiwasi.