kanga
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 1,025
- 494
Watoto wa shule za msingi za Serikali hususani katika Wilaya ya Temeke wamekuwa wakikosa masomo kama inavyotakiwa.Watoto hao mameku wakishinda uwanja wa Taifa kwa takribani wiki mbili sasa kwa ajili ya kuhudhuria mazoezi ya Alaiki na parade ya siku ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar itakayoadhimishwa hapo 26/04/20.Kitu muhimu cha kujiuliza muda wa kufidia masomo na vipindi walivyo kosa takribani mwezi mzima watapata wapi?, ingali wanafunzi wa shule zingine Tanzania wakiendelea na masomo yao kama kawaida?.Tabia hii ya kifsadi imeibuka hasa kipindi hiki cha Uongozi wa Kikwete ambapo wanafunzi wananyimwa haki yao ya kupata elimu na kuishia kuwa waburidishaji wanasiasa kwenye majukwaa.Matokeo mabaya na watoto wengine kushindwa kusoma na kufeli mitihani yao kwa kiasi kikubwa usababishwa na usanii huu ambapo viongozi wa elimu ngazi ya Wilaya,Mkoa na Taifa wanatoa kibali cha watoto kukosa vipindi na kufundishwa madarasani kwenda kujifunza kuwa waburudishahi wanasiasa majukwaani ambapo hata wanasiasa wenyewe watoto wao hawapo kwenye alaiki hizo.Shime wazazi wa watoto wanaosoma kwenye shule za Wailesi, Temeke,DUCE,Mgulani na hasa zilizokaribu na uwanja wa Taifa pingeni ukolono huu wa ajabu uluioota mizizi katika awamu hii ya Kikwete.Umwinyi na utumwa kwa watoto wetu wanaodhulumiwa kwa kukosa elimu bora wanazidi kukandamizwa kuwa watumwa kwa viongozi wa kisiasa hasa Kikwete.Maana baada ya sherehe za Muungano Kikwete na viongozi wengine uishia Ikulu na kusherrehekea lakini watoto wetu wanaendelea kutaabika kwa kukosa elimi kwa kipindi hicho.TUKATAE UTUMIKISHWAJI HUU NA UTUMWA.