Watoto wa wanasheria maarufu wa uingereza lakha na mucadam watua dar es salaam jumatatu

Watoto wa wanasheria maarufu wa uingereza lakha na mucadam watua dar es salaam jumatatu

so who

Member
Joined
Oct 28, 2011
Posts
73
Reaction score
7
watoto wa wanasheria maarufu wa Uingereza Lakha na Mucadam ambao nao wana kampuni yao ya uanasheria iliyosajiliwa kama Partners na wanasheria vijana maarufu kiTanzania wamefika jijini Dar es salaam kuja kusaidia kufungua kesi ya madai ya watumishi wa serikali za mitaa kutoka halmshauri mbali mbali nchini ambao wana madai ya madeni ya malimbikizo ya mishahara madai ya likizo uhamisho kupandishwa vyeo matibabu ambao hawajalipwa , na wakati wana vielelezo tosha na waliviwasilisha kwenye mamlaka husika kama madai yao serikalini wakapuuzwa.

Ili kuweza kuzishitaki halmashauri husika na serikali kuu kunyang'anya mali walizo nazo ili madeni hayo yalipwe kuna uwezekano mkubwa sana mali nyingi za halmshauri zikauzwa kutokana na maelezo ya awali ya vijana hao wa kihindi wanaozungumza kiswahili fasaha utafikiri wamekulia Kisutu.

Mmoja alisoma shule ya msingi Upanga akasema kwa mali za jiji la Dsm shule yake nayo inaweza uzwa ndipo nikamuuliza una shule hapa Dsm akanionesha kwenye mali zisihomashika ambazo halmshauri Dsm inamiliki ni pamoja na majengo ya shule akatania akasema huu mnada hizi zitauzwa fasta fasta ukiambiwa leo mnada shule ya muhimbili inauzwa mie ndio shule yangu hii wahindi wote Dsm utawaona hata ambao hujui kama ni wahindi watakuja na fedha hata kwenye mifuko ya rambo.

Hawa vijana wanaijua nchi hii utadhani wamezaliwa kituo cha mabasi Ubungo,nimekumbuka na kituo cha mabasi Ubungo nacho inaweza uzwa. Nikawauliza kama mtumishi anadai anaweza pewa hizi rasilimali badala ya deni lake akacheka akasema vipi unataka kupewa daraja la magomeni mwenzake akasema hapana lile ni la tanroads hii ni serikali kuu .

Kwa kifupi hawa baba zao ndio waliwatetea wakina Macghee kwenye kesi ya uhaini waliotaka kuipindua serikali sijui ilikuwa miaka gani ila ni wazuri na hataa wenzao wa kibongo wamewakubali kwamba watumishi wategemee ushindi baada ya muda si mrefu

orodha ya washitakiwa
katibu mkuu kiongozi
mwanasheria mkuu wa serikali
waziri wa tamisemi
wakurugenzi wa halmashauri kibao orodha ni ndefu.

Mpaka jana walikuwa wanahakiki mali zinaweza shikiliwa na ikishindikana halmashauri husika inazuiwa isifanye shughuli zake
icon6.png
 
Kwa nini mada hii isipelekwe kwenye jukwaa la sheria ikajadiliwe na wasomi wanasheria ili kuona kama ninachosemwa kinawezekana.
 
Back
Top Bottom