Watoto wa Wanasiasa na wakubwa wanavyobebwa na Bodi ya Mikopo

chakubimbi

Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
21
Reaction score
1
Watoto wengi wa wanasiasa na baadhi ya wakubwa wa nchi wamekua wakipewa mikopo na bodi ya mikopo ya elimu ya juu wakati hawana sifa za kupata mikopo hiyo. Wengi wa watoto hao huwa wanapewa scholarship nje ya nchi kupitia wizara ya elimu na wengine huwafata wazazi wao ambao ni mabalozi nje.

Mfano wa nchi ambazo hao watoto wa wanasiasa na wakubwa wengine wa nchi wamejazana ni Algeria, China, Cuba, Poland Urusi n.k wakiwa hawana sifa kwani wengi wao ni kidato cha nne au kidato cha sita waliofeli vibaya mno. Wakifika katika hizo nchi hupewa mikopo 100% ambazo ni mamilioni ya pesa za kitanzania.

Wengi wao wanapewa mikopo kwa wazazi wao kuwashinikiza watendaji wa bodi wawape mikopo watoto wao, Hii sio haki hata kidogo kwani watoto wa wakulima wanateseka bila kupata mikopo lakini watoto wa hawa wanasiasa wanapeta tu.

TANZANIA NI NCHI YETU SOTE .
 
Ungeweza kututajia na majina na nchi walizoko ingekuwa powa. Jf ni mahali pa ukweli na uwazi. Ukimwaga ugali kama Kagasheki watu wanamwaga mboga kabisa!
 
Nikweli kiasi fulani! yaani wale wenye uwezo wa kusomesha watoto wao ndio wanapewa mkopo wasiojiweza wanazidi kudidimia!!
 
Wa bongo mnapenda kupiga kelele sasa wewe mleta mada njoo na ushahidi weka hapa watu wajadili sio blah blah no research no rights to speak ukileta hoja lete na vielelezo tufanyie kazi
 
Mungu na atuponye watanzania, aitakase, ailinde na kuilinda nchi yetu, aikomboe na kuokoa na rushwa, uporaji wa rasilimali, kubaguana kwa misingi ya dini, chama, na ukanda, uvunjaji wa haki za binadamu na wanyama. Kila kona ni majanga tu, majirani wanatukimbia na kutubagua, wanzibari nao wameanza kumwagilia mbawa za kuruka, na sio ajabu baada ya kuruka wakajiunga na jirani zetu na kutuwekea vikwazo vya kiuchumi.

Kama tunanyanyasika ndani ya nchi kwa kunyimwa haki zetu, elimu jambo la msingi na la muhimu limejawa na siasa hata kuifanya elimu kudidimia. Haya huko nje nako wanatutenga, viwanja vya ndege twaitwa wabeba unga na wezi, je tuende wapi? tufanye nini?

Shime watanzania tujitathimini na kuangalia ni wapi tumekosea na kujirudi, then yafaa kuutafuta umoja wa kitaifa kwa kuisimamia amani bila kujali itakadi yeyote, kulinda rasimali za nchi hii bila kuwahurumia wahujumu uchumi, kuboresha elimu kwa kuithamini sekta ya elimu, kulinda heshima ya vyombo vya usalama na sio kuvifanya mtaji wa watu binafsi.
 

toa ushahidi na si kuleta swaga
 
hahahahaaa..cough,,cough..cough..yeye mwenyewe mtt wakigogo mdogo..sa cjui fungu la kumi limempita pemben kaamua kusalit kambi...
 
Mkuu wewe usiwaze kama vipi piga shule tu hapahapa bongo..kimsingi hizo hela wanazopewa na bidi ya mikopo sio nyingi kivileee...ni kawaida sana kwaio kama wewe sio wakishua kimtindo inaweza kula kwako maana hao wanapigwa tafu na wazazi wao imagine umemaliza chuo then una supp moja si tunaanza kutafutana ubaya kwenda kupiga supp na manauli ya donee(donation) na vitu kama hivyo..ni mawazo yangu tu hayo
 
YOTE TUMWACHIE MUNGU... but ukipata chance ucje ukawa kama wao kwa kulipiza kisas... soma uje ukomboe kizaz kijacho
 

Aamin!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…