Watoto waathirika wa Ubakaji, Ulawiti wanaumia Kisaikolojia, Ustawi wa Jamii na Mamlaka nyingine zinawasaidia inavyotakiwa?

Watoto waathirika wa Ubakaji, Ulawiti wanaumia Kisaikolojia, Ustawi wa Jamii na Mamlaka nyingine zinawasaidia inavyotakiwa?

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Wakati matukio ya ulawiti na ubakaji yakionekana kuongezeka nchini na Serikali kuwachukulia hatua baadhi ya watuhumiwa ikiwemo kuwafikisha kwenye Vyombo vya Sheria, lakini katika hali ya kusikitisha, vitendo hivyo vinaendelea kuacha maumivu yanayotokana na athari za Kisaikolojia kwa waathirika wa matukio hayo sambamba na Watu wao wa karibu ikiwemo wazazi, walezi ambao ushindwa kupata huduma ya Kisaikolojia kwa wakati.

Ripoti ya Jeshi la Polisi ya Mwaka 2023 ilibainisha matukio ya ubakaji 8,691, ulawiti 2,448, izingatiwe hayo ni yaliyoripotiwa uenda pia yapo ambayo hayakuripotiwa kwenye mamlaka hizo.

Ripoti hiyo ilionesha matukio ya ulawiti yaliyoripotiwa yameongezeka kwa kipindi cha kutokea Mwaka 2021, ambapo Ripoti ya mwaka huo ilionesha kulikuwepo na matukio 1,114.

Uchunguzi uliopatiwa jina la 'Uchunguzi wa Kizalendo' ambao ulianza kufanyika mapema kabla ya ripoti hiyo kutolewa, kwa kufanya udadisi mbalimbali ikiwemo kukutana mubashara na waathirika wanaodaiwa kufanyiwa vitendo, hivyo sambamba na Watu wao wa karibu, wengi wao wanadai kupitia hali ya changamoto ya kisaikolojia ikiwemo hali ya kujikatia tamaa.

Baadhi ya Wazazi na Walezi ambao ni waangalizi wa karibu na waathirika wa moja kwa moja wa matukio hayo nao wanabainisha wazi kuwa wamekuwa wakijikuta katika hali ya msongo inayotokana na vitendo ambayo wametendewa watoto wao hususani wadogo.

Katika udadisi huo wa Kizalendo', unabaini baadhi ya wazazi licha ya watoto wao kufanyiwa ukatili wa ubakaji na ulawiti, wengine ushindwa kuwaweka Watoto hao katika mazingira rafiki ya kuepuka kunyanyapaliwa, hususani kushindwa kuwahamisha Watoto hao kwenye mazingira ya Shule au kuwatoa kwenye jamii zenye taarifa juu ya vitendo vilivyotokea dhidi yao.

Sanjari na hilo uchunguzi huo unabaini baadhi ya Watoto wanaodaiwa kufanyiwa ukatili hasa wa ubakaji na ulawiti kujikuta mara kwa mara kwenye kizungumkuti cha kisaikolojia.

Ambapo inabainika mamlaka zimekuwa zikijikita zaidi kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watuhumiwa na huku nguvu ya kutoa msaada huduma ya Kisaikolojia yenye mwendelezo kwa waathirika wa ukatili huo ni duni ikiwemo kushindwa kuwafikia ipasavyo waangalizi wa karibu wanaomzunguka Watoto ikiwemo wazazi na walezi.

Kutokana na udadisi wa kizalendo unabaini hali hiyo imekuwa ikiwaacha na maumivu ya kisaikolojia Watoto wengi wanaofanyiwa vitendo hivyo sambamba na waangalizi wao wa karibu, jambo ambalo baadhi ya Wazazi wanabainisha kuwa hali hiyo imekuwa ikipelekea waathirika wa moja kwa moja ambao ni Watoto kupolomoka kwenye kimasomo kutokana kupoteza hali ya kujiamini, kutokana na mazingira yanayowazunguka.

Hata hivyo, inafahamika kwenye jamii kuna Maafisa Ustawi wa Jamii sambamba na Madawati ya Kijinsia hususani Watoto kwenye baadhi ya vituo vya Polisi, lakini uchunguzi unabaini bado wengi wao ushindwa kutoa msaada endelevu hasa wa Kisaikolojia kwa wanaoathirika na matukio hayo sambamba na watu wa karibu.

Hali hiyo inabainishwa na baadhi ya waathirika ambao wamewahi kuripotiwa kukumbana ukatili wa aina hiyo na kuripoti kwenye mamlaka hizo.

Uchunguzi wa kizalendo unabai kuwa jambo hilo limekuwa likichangia changamoto kwa baadhi ya Wazazi na Walezi, ambao ni waangalizi wa karibu wa waathirika wa moja kwa moja, ikiwa ni kutokana na kupata ugumu wa kuwajenga kisaikolojia watoto hao, hali ambayo wengi wao wanadai inawapelekea nao kujikuta kwenye msongo wa mawazo wa mara kwa mara.

Kufuatia uchunguzi huo hasa kwa kuzungumza na baadhi ya wadau ikiwemo wanasaikoloja, inabainika athari zinazowapata Watoto waliofanyiwa ukatili wa aina hiyo harafu wakakosa msaada wa huduma ya kisaikolojia ni kubwa kwao binafsi, kwa jamii na Taifa kiujumla.

Miongoni mwa madhara yanabainishwa ni pamoja na Watoto hao kupoteza hali ya kujiamini, kutofanya vizuri kwenye masomo, kuchukua uamuzi usio rafiki, kujenga mioyo wa chuki na visasi ambavyo uathiri maisha yao hata wakishakuwa mkubwa.

Wito wa ‘Mzalendo’
Ni muhimu mamlaka kuwajengea uwezo maafisa Ustawi wa Jamii Madawati ya Jinsia na Watoto kwa kuwawezesha nyenzo muhimu mbalimbali zitakazowafanya kuwatambua waathirika na kuwapatia huduma za kisaikolojia kwa utaratibu rafiki.

Ikizingatiwa katika uchunguzi huu nabaini asilimia kubwa ya watoto wanaokumbwa na ukatili wazazi na walezi wapo katika hali duni ya kiuchumi jambo ambalo wanakili kuwa ni vigumu kwao kumudu gharama za WanasaikolojIa binafsi huku wengine wakiwa hawajui kabisa namna wanavyoweza kuwafikia.

Hata hivyo pia kutoka na hali inayobainika, ni muhimu Serikali isihishie kuwawajibisha watuhumiwa wa ukatili, badala yake ijenge utamaduni kuwapatia mazingira rafiki Watoto walioathirwa na ukatili ikiwemo kielimu na kijamii ili kuwaepusha na athari mbalimbali ikiwemo kunyanyapaliwa.

Soma: Mwaka 2023 kulikuwa na Makosa 37,448 ya Ukatili wa Kijinsia Tanzania, 15,301 yalikuwa kwa Watoto
 
Kwa hali ilivyo kwa sasa. Ni ukweli kwamba karibu kila Mtanzania anahitaji mwanasaikolojia.
 
Wakati matukio ya ulawiti na ubakaji yakionekana kuongezeka nchini na Serikali kuwachukulia hatua baadhi ya watuhumiwa ikiwemo kuwafikisha kwenye Vyombo vya Sheria, lakini katika hali ya kusikitisha, vitendo hivyo vinaendelea kuacha maumivu yanayotokana na athari za Kisaikolojia kwa waathirika wa matukio hayo sambamba na Watu wao wa karibu ikiwemo wazazi, walezi ambao ushindwa kupata huduma ya Kisaikolojia kwa wakati....
Hii Dr Gwajima ataijibu kule kwenye wizara yake ,mod wataipeleka huko soon.
 
Back
Top Bottom