JF kuna mbaba amefiwa na mwenzake some 2 years ago..ana watoto wakubwa age between 12-16 (three of them), wanamkataza huyo mbaba asioe...alipojaribu kuwa-introduce hiyo issue watoto hawataki??
mzee yuko between 45-56 years of age. hii imekaaje...vipi watoto siku hizi wana mamlaka..jamaa anampango wa kuwapeleka wote boarding schools wakirudi likizo wanamkuta mama yao mdogo..what do you think???
Hakuna mali za kihivyooo..just average earning (working class)..mawazo yao ni manyanyaso unajua hizi film za ki-nigeria ..asewapeleke shule ili apata nafasi ya kuoa ila awapeleke shule ili waache kumtegemea, watoto wanahisi akioa mali zote zitakuwa chini ya mama yao mdogo.
Nakubaliana nawe kwa sehemu kubwa watoto wanamuitaji baba yao wakati huu kuliko wakati wowote, atakuwa amefanya kosa kubwa kuwapeleka boarding ili tu yeye apate kuoa. Jambo la kufanya ni kuendelea kuwafahamisha umuhimu wa yeye kuoa, huku akiwaonyesha kuwa hatakuwa mbali nao. Maana tofauti na inavyoweza kuonekana hawa watoto wala hawakatai baba yao kuoa kwa ajili ya mali, bado ni wadogo kuthamini mali kiasi hicho, kinachowasumbua ni security yao. Kama baba atatumia hekima ambayo itawafanya wajenge imani kuwa hawatakuwa peke yao baada ya baba yao kuoa, hawatakuwa na taabu.bond baina ya watoto na mzazi ni muhimu sana. ingawa hao watoto ni wadogo lakini nadhani si vyema kuwakimbiza kwani wanaweza wakamchukulia baba yao vyengine na hivyo kusababisha mapenzi yao kupungua kwa baba yao. kwavile hao watoto ni wadogo nadhani angewatumilia ujanja wa kuwalainisha kwa vizawadi na ajaribu kuwafahamisha umuhimu wa yeye kuwa na mwenza . inawezekana watoto wana kasumba ya kwamba kila mama wa kambo ana mateso, hivyo pia awathibitishie usimamizi wake kwao kwamba hawatateseka na atakuwa nao bega kwa bega kuhakikisha mapenzi baina yao na mama mpya.
ni ushauri wangu tu. kama mbovu tia kwenye taka.
quiet
Inavyoonekana hao watoto eitha walishaona watoto wenzao wanavyonyanyasika na mama wa kambo,au wameshaona filamu ambazo zina parts ambazo kuna manyanyaso,sasa hiyo naona kama vile imewa-affect na wanahisi kuwa labda mama atakaeletwa hapo nyumbani anaweza kuwanyanyasa.
Nionavyo hao watoto wanatakiwa wapate ushauri kuwa sio kila mama wa kambo ni mnyanyasaji.
....Yawezekana watoto wameona mama mwenyewe ni mjasiria mali sana anaweza kumfilisi baba yao na wao wakalost jumla..So they are right...reaction ya watoto inategemea sana na mama mwenyewe!!! akina mama wengine hapendi kuwalea watoto wa mke mwenzake aliyetangulia!!!Huyo mwanamke pole yake, watoto wameshaanza kuonyesha chuki mapema kwa mama wa kambo kabla hajafika.
Muhimu huyo baba inabidi awakalishe chini na kuwaeleza umuhimu wa yeye kuwa na mke na wao kuwa na mama mlezi. Maana nyumba bila mwanamke bado haijakamilika.
na huyo mama akiingia ndani ya hiyo nyumba awe mpoleasilete ukorofi wa kimama kambo la sivyo ataipata joto ya jiwe
kuna wanawake wengine hawapendi kulea vizuri watoto wa wanawake wengine
na hivo vitoto vinaonekana vilikuwa na mapenzi mazito na mama yao vina ufahamu mkubwa sana
Baba atumie muda mrefu kuongea na watoto wake na kwa upole na imani watakubali asifanye kitu cha ghafla
Ngojeni amlete huyo mwanamke halafu azae mtoto wa kwanza muone! Mama wa Kambo si MAMA
Kila kitu mbona anasingiziwa ibilisi?? Si Yeye! Bali Kiburi,. Akishazaa ndo atajiona amefika!Mnyanyaso kwa watoto wa kambo Kwenda mbele! mimi kama huyo mwanaume nafunga kizazi changu! eti? si watoto tayari nakuwa ninao???yaani huwa nashindwa kuelewa huwa ni Ibilisi anawaingilia au??
Ngojeni amlete huyo mwanamke halafu azae mtoto wa kwanza muone! Mama wa Kambo si MAMA
hapo kwenye red mkuu si mama ni nani????? Acha jazba
hapo kwenye red mkuu si mama ni nani????? Acha jazba