Watoto Wananisumbua: Wanagombana Sana


Masihara hayo, utingo, yasije yakakukuta yaliyonikuta, mweee!
 
Jamani wanajf naomba tumsaidie rafiki yangu. Huyu rafiki yangu ana watoto wake wawili wanaopishana mwaka tu kati yao, mmoja ana miaka mitatu na miezi 11 na mwingine ana miaka miwili na miezi nane..

Mkuu hao watoto bado wadogo..muombe rafiki yetu aache kutembeza bakora kwani sio vizuri. Pili muombe asitafute kizingizio cha kutorudi nyumbani mapema kukimbia kelele za watoto...Nina timu zaidi kidogo ya hiyo ambayo ilinipa kazi ya kutunga sheria ya kuangalia katuni yaani kila mtu ana muda wake...baada ya kuchoka kuwa referee wa ngumi kila siku..

Kuhusu kupigana kwa hao watoto nadhani ni dalili nzuri kuwa hao watoto kichwani wako active sana..hivyo hawawezi kutulia..ni ushindani wa kiakili zaidi kuliko Physical...Huko kupigana ni impact ya mambo yanayoendelea kichwani. Kikubwa ndugu yetu atafute interest za hao watoto..kumbuka watoto wanapishana interest..afanye "try and error" ..mpaka ajue interest zao ambazo zitafanya akili iwe busy na kuacha kufikiri kugombana..
 
Watenge kwa kuwaweka kwenye kona.watoto hawapendi kutengwa.kila mmoja muweke kwenye kona yake.watapunguza
 
Pia jaribu kuangalia selection ya games na toys unazowanunulia ziwe zenye michezo shiikishi; kila mmoja awe anamuhitaji menzake ili kufurahia mchezo!
 

ni kawaida, mtu akiwa na mtoto mmoja anakuwa mzazi, wakiwa watoto wawili anakuwa refarii
 
Pengine toto moja cyo damu yake!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…