Watoto wengine presha tupu!✔

Bishop Hiluka

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
7,147
Reaction score
14,699
Baba na mama baada ya kurudi safari pamoja wakakuta BARUA iko mezani SEBULENI ikisema:

"Baba na mama, ni matumaini yangu kuwa mtasoma ujumbe wangu huu kwenye karatasi niliyoiweka
juu ya meza, naomba msishtuke mana ni mambo ya kawaida kwenye maisha tunayoishi, najua mtaumia kwa vile bado nasoma na ndiyo nipo kidato cha kwanz…

Napenda kuwajulisha kwamba sasa hivi mnaposoma hii barua sipo nyumbani, nimetoroka maana nimegundua
nina uwezo wa kujitegemea kwa sababu mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 13 na ninajua kipi chema na kipi kibaya.

Tangu mwezi mmoja uliopita nilikuwa na uhusiano na binti mmoja aliyeitwa Rachel, mwenye umri wa miaka 27 na kwa sasa
ndio naishi naye kwenye chumba alichopanga. Nilipokuwa nyumbani sikuwa napata hela za kutosha ila sasa nimeanza kushika noti za shilingi 10,000… Msichana niliyenaye ni mzuri sana wa umbo na ninampenda sana, amenifundisha njia za kutafuta hela.

Amenipangia kazi ya kuuza dawa za kulevya na yeye ikifika
usiku anaenda kuuza mwili wake, basi kila siku tunapata hela ya kutosha, huyu mchumba wangu ni msichana mwenye bidii, kwa siku analala masaa 6 tu maana mwanaume yeyote akija lazima awe naye
chumbani kwa muda wa masaa 3.

Msiwe na hofu, nipo salama kabisa na nimeamua kumwoa Rachel maana ni kila kitu kwangu. Pia amenunua gari la kubebea mbao kwa hiyo biashara inaenda vizuri.

Rachel ameenda kupima afya na amekutwa na upungufu wa kinga
mwilini, mara nyingi namridhisha anapotaka kitu flani, iwe kufanya naye mazoezi ya viungo au kufanya naye mapenzi, si mnajua unapokuwa na mgonjwa unakuwa naye karibu.

Ila mimi pia sijihisi vizuri maana kila saa nakohoa tu na sina uhakika kama nimeambukizwa. Tumepanga baada ya miaka miwili tutawatembelea, nadhani mpaka miaka miwili iishe atakuwa
ameshajifungua, na ni furaha yangu mtamwona mjukuu wenu. Wazazi wangu, sina la kuongeza kwa herini. Mungu
akipenda tutaonana.

NB:

Baba na mama, mimi nipo chumbani kwangu najisomea,
mnachokisoma ni home work ya mwalimu wa Kiswahili alituambia tutunge hadithi fupi ya kusisimua, naomba muiangalie kama kuna
makosa!"

😡 😵 🙄 😳 😱 🙁 🙁
 
Wazazi wakazimia kabla ya kumalizia stori
 
Hahaha.........umekill kijana
 
Na shule yenyewe namwachisha hawezi kinitia presha namna hiyo mimi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…