Watoto wetu katika taasisi za elimu hufundishwa nidhamu ya uoga na unyenyekevu kw watawal

Watoto wetu katika taasisi za elimu hufundishwa nidhamu ya uoga na unyenyekevu kw watawal

bbukhu

Member
Joined
Feb 25, 2012
Posts
58
Reaction score
1
Taasisi za elimu kawaida ni mahali ambapo wanafunzi wangepaswa wafundishwe uzalendo.Lakini katika nchi yetu hali ni tofauti kwani wanafunzi hufundishwa uoga na unyenyekevu kwa watawala. Hawafundishwi uzalendo.
Natoa mfano moja: Nilipokuwa kidato cha sita nilisimamishwa shule kwa muda wa miezi mitano kwa sababu niliandika barua ya maoni katika gazeti la habari leo kuhusu matatizo sugu yaliyokuwa yanaikabili ile shule yetu. Ile barua ilisomwa katika redio moja zaidi ya mara mbili na walimu wangu akiwemo heamaster walisikia. Hiyo ndiyo hali halisi. Ipo mifano mingi sana. Wapo wanachuo wengi sana ambao wamefukuzwa na wengine kusimamishwa masomo kwa sababu ya kudai haki zao. Kwa hiyo katika nchi yetu wanaodai haki huchukuliwa kama waasi na wanaovunja sheria za nchi.Na wale watenda maovu huchukuliwa kuwa watu wazuri na wenye uzalendo. Kweli hali hii itaendelea hadi lini? Kwa sasa tanzania ina wataalamu wengi ambao wako nje ya nchi kwa sababu ni wapinga maovu ya watawala kwa hiyo wao huchukuliwa kuwa ni wahaini.
 
Back
Top Bottom