Nimeona mambo mengi ila mengine ni aibu hata kuyasema ilihali wale wanayoyafanya wanaona ni sawa na kawaida tu God forbid
Watu wanafanyiana kicheni pati wajue jinsi ya kulea mume wanasahau watoto.Inabidi sasa ianzishwe sebuleni pati sijui!But seriously...kungekua na semina za kuelimisha watu athari za unyanyasaji wa watoto ingesaidia kwa kiasi fulani!
Kila siku tunaongelea mapenzi tunasahau watoto....embu leo tuwe kifamilia zaidi.
Leo kuna kipindi nlikua naangalia kikanisikitisha sana.Kuna mwanamke yeye anamwadhibu mtoto wake kwa kumnywesha pilipili na kumuogesha maji baridi kabisa...wakati mwingine eti anamlisha sabuni.
Nikakumbuka wakati nakua kuna mtoto wa jirani yetu yeye alikua naishi na babu yake, siku moja aliachwa nyumbani alafu akaenda kucheza....babu yake alivyorudi alichofanya ni kumchapa alafu akamweka kwenye gunia lenye yale majani yanayowasha alafu akamtundika wakati chini moto unawaka.Yule mtoto alitoka mwekundu kama nini sijui....sikumbuki kama kuna jirani aliyethubutu kumkemea yule mzee.Nyingine tuliwahi kua na msichana wa kazi ambae alikua na mtoto wa zaidi ya mwaka mmoja.....ilikua tukiwa shule yule dada anamfunga mtoto wake kwenye mguu wa kitanda ili eti asimsumbue.Yule mtoto analia na kukojoa pale pale mpaka analala...tukirudi basi tunakakuta kamelala uvunguni.Anagombezwaaa ila tukiwa hatupo tu anafanya vile vile.
Bila kusahau wale watu wanaoishi na watoto wa wenzao pamoja na wa kwao alafu wanawatreat fofauti.Kuna baadhi ya ndugu zangu nimewahi kuishi nao wa aina hiyo.....unakuta wale watoto wasio na mtu wa kumlilia wananyanyaswa ila wale wakwao na wale wenye ndugu au wazazi wao wenye uwezo wanalelewa vizuri tu.
Na yule aliyevutwa nyusi na mwalimu mpaka macho yakageuka!!
Kusema kweli hizi hali zote zinasikitisha.Kuona mtu mzima anamnyanyasa mtoto kwa sababu yoyote ile na kwa kisingizo chochote kile haifai.Wengi wao hawana wa kumlilia na kushtaki sio kitu ambacho kinaweza kufanyika kirahisi kwasababu kitendo cha kumpeleka mzazi au ndugu anaekulea kwenye vyombo vya sheria mara nyingi itaongeza matatizo zaidi ya kupunguza..
Naomba niwaombeni wanajamii tuwe na huruma jamani.Awe mtoto wako...wa ndugu au jirani jaribu kutokua mnyanyasaji.Kama mzazi kua na ukaribu na mwanao ili hata kama kuna mtu mwingine anaemnyanyasa iwe shuleni, mtaani au nyumbani iwe rahisi kukwambia.Na kwa wale ambao wanaishi na watu ambao sio wazazi halisi wa wanao (mama na baba wa kambo) kua na tabia ya kuongea na mwanao kujua mambo yanayoendelea nyumbani ukiwa haupo.
Mateso ya utotoni hua yanaacha makovu mabaya sana....JALI NA KUA NA HURUMA huo ndo ubinadamu!
Sipiyu tatizo sio wanachofanya au wanachosema ila ni adhabu tunazowapa!Kuna picha nimeona jana mtoto ameungua matakoni kwa kukalishwa kwenye jiko la mkaa!Hata kama huyo mtoto angekua ameua bado hastahili adhabu ya aina hiyo!Besides..mtu kama huyo aliyekutwa akiandika mambo ya kimapenzi alitakiwa kukalishwa chini akaelezwa kosa lake lilipo bila kusahau uwepo wa mzazi wake pale.Kuna mwl aliwahi kumchapa mwanafunzi mpaka mkono ukachanika..japo sikumbuki kosa lake ila nna uhakika halikua kubwa!
Lizy umeniudhi sana! basi tu sina chakukufanya! Mada ni nzuri sana lakini umeisemea kama wewe unapenda hao watoto wateseke! Umesema wanaotesa watoto (wazazi wakipelekwa mbele ya sheria ni kuongeza matatizo?) Kwa hiyo wewe unafikiri ulivyoshauri hapa jamvini ndo taarifa zimewafikia walengwa?? hujui wanaoteseka wako kijijini au mijini ambao hawajui hata maana ya jamii forums hata ukimwambia internet anakwambia umenitukana!!! Una kitu serious sana ambacho mtu akisoma tu anapandwa na uchungu hapa ni kutafuta njia ya kuwasaidia hawa watoto! Tukisema kila mtu aweke story moja ya hivyo hapa jamvin mpaka utalia machozi! mimi umenihukiza kwa sababu ya lugha ya upoleeeeeee wakati unazungumzia kifo! Sasa basi mimi nimekasirika naanzisha kampuni ya kusaidia hawa watoto! ngoja sasa:embarassed2:
Meja ni wachache sana kwenye jamii yetu wanaoweza kukaa chini na kusoma kitabu kuhusu watoto!Baba yuko baa..mama yuko bize hata muda hana!Ni kweli ila tatizo ni kwamba watu hatusomi vitabu na pia hatutaki kujifunza kutokana uzoefu. Kuna vitabu vingi sana vinaeleza jinsi ya ku-deal na watoto wa umri tofauti. Pia kuna suala la migongano kwenye ndoa pale anapopatikana mtoto wa kwanza. Inabidi tujitahidi kujisomea pia.
Well ni shida ya familia nyingi za kikwetu kuwabagua watoto wasiokuwa wa familia ile; mie nilikuwa likizo napita kwa ndugu yangua ambaye alikuwa na watoto wa umri wangu; basi jioni akirudi na zawadi aaingaia nazo chumbani na wanawe wanagawiwa huko na kama ni matunda utaambulia kuona maganda yakitoka chumbani.........na kuna wakati nilikuwa nazuiwa likizo nyingine nisiende hapo kwani hakuna nafasi.......
Ukweli ni kwamba familia nyingi zinapata watoto bila utayari wa kuelea hao viumbe......
Hongera Lizzy...using ya head rightly