SoC02 Watoza kodi ni wezi na wanyang'anyi wazoefu

SoC02 Watoza kodi ni wezi na wanyang'anyi wazoefu

Stories of Change - 2022 Competition

Kasiano Muyenzi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2018
Posts
13,858
Reaction score
22,729
Tangu enzi na enzi ulimwenguni kote inasemekana watoza kodi ni watu wa kujinufaisha binafsi, hutumia mbinu nyingi kuchota na kujinufaisha wao binafsi, na kwa kawaida hupata utajiri mkubwa kupitia kodi

Katika Biblia Luka 19:1-10 kuna simulizi ya Zakayo mtoza ushuru (nitasimulia kwa ufupi kwa faida ya wasiomjua)

Zakayo alikuwa mkuu wa Watoza ushuru (chief tax collector)alikuwa tajiri sana na alijulikana kwa wenyeji wa mji wa Yeriko kuwa ni mtu asiyefaa. Ilitokea siku moja Yesu aliingia katika huo mji Zakayo alikuwa miongoni mwa watu waliijitokeza kumwona Yesu lakini kutokana na umati uliomzunguka Yesu kuwa mkubwa alishindwa kumwona maana alikuwa ni mtu mfupi, hivyo alitumia mbinu ya kupanda juu ya mti ili Yesu akipita hapo chini ya mti aweze kumwona. Baada ya Yesu kupita katika huo mti jambo la kwanza alilofanya Yesu ni kumtaka Zakayo ashuke chini na waongozane nyumbani kwake maana ni mgeni wake. Watu walinung'unika kwa Yesu kuingia nyumbani kwa Zakayo.

Sababu ya watu kunung'unika ilikuwa kwamba walimjua vyema Zakayo kwamba ni mtu mwenye "dhambi" asiye faa ni mnyang'anyi.

Baada ya Yesu kuingia ndani, Zakayo alifanya uamuzi wa kushangaza!
Zakayo alifanya uamuzi ambao ulimuondolea hatia zote zilizomhusu katika kazi yake ya utoza ushuru, uamuzi wake huo ulibeba mambo mawili.

1. Kugawa nusu ya mali yake kwa maskini.

Alitoa mgao kwa watu masikini pekee.

2. Kumrudishia mara nne yeyote aliyemnyang'anya kitu.

Alijua fika kuwa katika ukusanyaji wa kodi alinyang'anya mali za watu kwa faida yake binafsi hivyo aliamua kuachana kabisa na unyang'anyi kwa kurudisha mali na fidia juu.

Zakayo aliamua kuachana na uovu kabisa.

Turejee katika mada yetu.
Watoza kodi wanajinufaisha binafsi kwa kuiba kodi zetu. Tunajua fika kuwa kodi tunalipa ili taifa letu liwe na maendeleo katika nyanja zote, kodi zinalipwa lakini hatuoni maendeleo kwa kuwa Wakusanya kodi ni wezi wakubwa .

Walipa kodi ambao wengi wao ni raia maskini wanateseka sana hasa maeneo ya vijijini na baadhi ya maeneo ya mjini, tena watoto wao wanapata elimu duni kabisa, shule wanazosoma watoto wa walipa kodi masikini huwezi kuta mtoto wa mtoza kodi anasoma huko kwa kuwa ni duni hata wao wanalijua hilo ndio maana wanabidii ya kuiba ili wajinufaishe wao kwa kuwasomesha wana wao na wote wa familia zao katika shule za gharama ya juu.

Tangu enzi ya mkoloni kodi ililipwa hadi leo inalipwa. kuna matunda ya kodi yaliweza kuonekana katika utawala wa awamu ya kwanza kwa sababu waliopewa dhamana ya kusimamia makusanyo wengi wao walikuwa wazalendo na waadilifu wenye hofu ya Mungu. Baada ya awamu hiyo kupita awamu zilizofuata zilitengeneza mazingira ya kuwapata wezi wa kodi ambao wametufikisha hapa tulipo.

Kwa wakati huu wa sasa viongozi waadilifu na wazalendo wa kweli hawapo kabisa.

Kodi zetu zinatumika kinyume na malengo, zinawanufaisha zaidi Watoza kodi walio wezi na wanyang'anyi

Malalamiko ya walipa kodi yapo mengi sana na yanasikika kila kona ya nchi lakini hakuna mwenye dhamana ya uongozi anayeweza kuchukua hatua kwa kuwa kila mmoja (kiongozi) ni "mbuzi" anayekula kwa urefu wa kamba yake.

Watoza kodi wetu wanaweza kwa Zakayo mtoza ushuru ambaye aliposikia manung'uniko ya watu juu ya "dhambi" zake alifanya uamuzi mawili kama nilivyoelezea hapo juu na uamuzi wake wa kwanza ukawa ni kutoa nusu ya mali zake kwa masikini!

Itakuwa vyema sana kwa Watoza kodi wa nchi yetu wakifanya maamuzi kama ya Zakayo kwa kuacha wizi na pia watoe nusu ya mali zao kuwawezesha watoto wa walipa kodi masikini wapate elimu bora na maendeleo kwa ujumla sawa na wanayopata watoto wao.

Kwa sasa wanajifanya wana kazi nyingi za kusimamia ukusanyaji wa Tozo lakini kelele na manung'uniko ya walipa kodi maskini yamekwisha kusikika kila mahali, yaani Tozo zinawaumiza sana mwananchi masikini Ila zinanufaisha Wakusanya kodi pekee, kwa maana ya kwamba mkusanya kodi ataitumia Tozo atakavyo mwenyewe.

Kwa mfano akitaka kutumia gari la kifahari au kujilipa mishahara ya wafanyakazi hewa ama kufanya vitu vyote vya anasa kwa manufaa yake binafsi atafanya tu.

#Manung'uniko ya watu wa Yeriko yalimfikia Zakayo mtoza ushuru kwamba ni mtenda "dhambi", na Zakayo alijiongeza wala hakuufanya moyo wake kuwa mgumu bali alichukua uamuzi wa kuachana na "dhambi " hizo na alizitaja kabisa akalipa na fidia.

Itafaa sana watoza Tozo wakijifunza kwa Zakayo mtoza ushuru

Kwa Tanzania wizi kupitia mapato ya kodi unasimamiwa vizuri sana na hao wezi, hivi kweli wanasubiri kufutwa kazi au wanasubiri kufa ndio waache huo wizi?
Ni bora wakichukua uamuzi kama wa Zakayo mtoza ushuru watakuwa wapendwa kwa Mungu maana hata Zakayo alipochukua uamuzi aliingia ktk historia njema tena alipendwa mno.

Watanzania wamechoka kwa kukamuliwa

Manung'uniko hayataisha hivyo basi watu wenye dhamana mliodhamiria kujichotea kodi kwa manufaa yenu binafsi niwashauri tu kuwa kama mtasikia majina yenu yanatajwa sana na wananchi kwamba nyie ni wezi na mmebuni "Tozo" ili muibe kiulaini ni bora mkicha mara moja! Fanyeni maamuzi kama ya Zakayo mtoza ushuru kwa kurudisha vyote mlivyoiba.

Mwisho niwape tahadhari kuwa msijione kuwa wajanja kwa kuiba jasho la walalahoi, siku zote jasho la mtu halipotei bure ipo siku mtaumbuliwa, kama sio nyie basi ni vizazi vyenu mtakavyovirithisha hizo mali za wizi.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom