DOKEZO Watoza ushuru stendi ya mabasi Magufuli hawatoi risiti hivyo kuikosesha mapato manispaa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest

Kumekuwa na vitendo vya ufisadi unaofanywa na baadhi ya watumishi wa manispaa ya Ubungo kitengo cha wakusanya ushuru pale stendi ya mabasi Magufuli.

Wakusanya ushuru Hawa kwa kushirikiana na wasimamizi wao wa stendi pamoja na baadhi ya watumishi makao makuu Ubungo manispaa kitengo cha fedha na uhasibu wamekuwa wakichukua pesa bila kutoa risiti kwa wananchi au wateja wao na mwisho wa siku kugawana mapato hayo.

Nashauri ofisi ya Raisi TAMISEMI ilifanyie jambo hili uchunguzi wa kina na hatua zichukuliwe kwa wahusika.

Pia soma ~ Miundombinu ya mabomba kwenye Vyoo vya 'Magufuli Bus Terminal' imeharibika, maji yanatoka hovyo na hakuna anayejali
 
Inasikitisha sana lakini hakuna namna maana walishaambiwa wale kwa urefu wa kamba zao
 
Hii ndio Tanzania ninayoifahamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…