TAWA
JF-Expert Member
- Jun 23, 2013
- 3,674
- 1,572
Naripoti kutoka Morogoro manispaa:
Kumekuwa na changamoto kwa wakazi wa manispaa ya Morogoro kutozwa ushuru wa maegesho ya magari na watu wa halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kinyume na utaratibu.
Ukiegesha gari bila kujali katika maegesho rasmi ya Manispaa au popote pale anakuja mtu wa Manispaa na mashine na kuipiga picha gari na kukuandikia deni bila kukupa control number ya kulipia au kukueleza chochote kuhusiana na malipo hayo. Utakuja kuuona malipo siku ukija kusimamishwa na kukaguliwa madeni ndipo utaona kuwa Una madeni mengi ya ushuru wa maegesho.
Kilicho kibaya zaidi, watu hawa wanachaji maegesho mpaka kwenye nyumba za watu au sehemu za kutolea huduma binafsi kama vile kwenye migahawa, bar au hospital japo watoa huduma hizo wameweka maegesho kwa ajili ya wateja wao.
Soma Pia: Ushuru wa maegesho umegeuka kuwa wizi usiotumia mabavu wa serikali dhidi wananchi wake
Nadhani huu ni utapeli unaopaswa kupigwa vita kwani kuwa na gari siyo laana katika taifa hili.
Ushauri wangu kwa Mkurugenzi, atengeneze maegesho rasmi ya magari mfano Ile stendi ya zamani pale mjini Kati, soko kuu la Kingalu stendi ya Msamvu na maeneo yanayofanana na hayo. Hapo ni halali kwake kuchaji ushuru wa maegesho na siyo kwenye majumba ya watu.