Watu 10 matajiri zaidi Duniani

Watu 10 matajiri zaidi Duniani

Mamujay

Senior Member
Joined
Dec 24, 2022
Posts
149
Reaction score
345
Kupitia jarida la World of Statistics limetoa orodha ya watu matajiri zaidi duniani au Mabilionea wa Wakati huu kulingana na Forbes, wameeleza kuwa Elon Musk ameondolewa namba moja kutokana na hasara aliyoipata mwaka 2022.
Jukwaa hilo la kufuatilia utajiri linatoa masahihisho yanayoendelea kuhusu thamani halisi na cheo cha kila mtu aliyethibitishwa na Forbes kuwa bilionea.

Hutokana na Thamani ya hisa za watu binafsi husahihishwa kila baada ya dakika 5 masoko ya hisa yanapofunguliwa tu.

Kwa mwaka huu 2023 hii ndio orodha ya watu 10 matajiri zaidi duniani, katika watu hao mabilionea 6 wanatoka Marekani.

1. Bernard Arnault:

Ni mfanyabiashara mkubwa kutoka nchini Ufaransa, mwekezaji kwenye sekta za sanaa. Yeye ndiye mwanzilishi, mwenyekiti, na afisa mkuu mtendaji wa LVMH Moët Hennessy, Louis Vuitton, kampuni kubwa zaidi ya bidhaa za anasa (luxury) duniani. Utajiri wake unakadiriwa kuwa ni $190b

2. Elon Musk:

Ni mfanyabiashara mkubwa na mwekezaji mzaliwa wa Afrika Kusini kwa sasa akiishi nchini Maarekai, Yeye ndiye mwanzilishi, Mkurugenzi Mtendaji na mhandisi mkuu wa SpaceX; Mkurugenzi Mtendaji na mbunifu wa bidhaa wa Tesla, mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa Twitter, mwanzilishi wa The Boring Company; mwanzilishi mwenza wa Neuralink na OpenAI; na rais wa philanthropic Musk Foundation. Utajiri wake unakadiriwa kuwa ni $146b

3. Jeff Bezos:

Huyu ni mjasiriamali wa Kimarekani, mmiliki wa baadhi ya vyombo vya habari, mwekezaji, na mwanaanga wa kibiashara. Yeye ndiye mwanzilishi, mwenyekiti mtendaji, na rais wa zamani na Mkurugenzi Mtendaji wa Amazon.Utajiri wake uakadiriwa kuwa ni $120b

4. Gautam Adani: Utajiri wake unakadiriwa kuwa ni $113b

5. Bill Gates: Utajiri wake unakaridiwa kuwa ni $111b

6. Warren Buffett: utajiri wa zaidi ya dola bilioni 110 kufikia Januari 2023, na kumfanya kuwa mtu tajiri zaidi wa sita ulimwenguni.

7. Larry Ellison: Utajiri wake unakadiriwa kuwa ni $100b

8. Larry Page: Utajiri wake unakadiriwa kuwa ni $89b

9. Steve Ballmer: Utajiri wake unakadiriwa kuwa ni $86b

10. Carlos Slim: Utajiri wake unakadiriwa kuwa ni $85b
 
Back
Top Bottom