Watu 11 wauawa katika mlipuko kwenye mkutano wa M23

Watu 11 wauawa katika mlipuko kwenye mkutano wa M23

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Watu 11 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa Alhamisi wakati wa mlipuko katika mji wa mashariki mwa Congo wa Bukavu uliotokea kwenye mkutano wa hadhara ulioongozwa na viongozi wa kundi la M23, ambalo lilichukua udhibiti wa mji huo mapema mwezi huu.

Viongozi wa waasi wameituhumu Serikali ya Congo kwa shambulizi hilo la bomu na kusema washambuliaji ni miongoni mwa waliouawa katika mlipuko huo, huku kukiwa ripoti za kukinzana kati ya waasi na maafisa wa eneo hilo kuhusu idadi ya washambuliaji na waathirika.

Rais wa Congo ameyatuhumu “majeshi ya kigeni” ambayo hakuyataja kuhusika na shambulizi hilo.

“Shambulizi hilo lilisababisha vifo vya watu 11 na uchunguzi unaendelea. Muhusika wa shambulizi hilo ni miongoni mwa waathirika,” Corneille Nangaa, kiongozi wa muungano wa Congo River Alliance (AFC), ambao unajumuisha M23, aliwambia waandishi wa habari.

“Kuna watu 65 waliojeruhiwa, sita kati yao wako katika hali mbaya na wanapewa matibabu katika chumba cha upasuaji.”

Viongozi wa M23, akiwemo Nangaa walikuwa wanakutana na wakazi wakati mlipuko huo ulipotokea mjini kati Bukavu.

M23 imeitumu serikali ya Congo kwa kupanga shambulizi hilo.

Rais Felix Tshisekedi amelitaja shambulizi hilo kama “kitendo kibaya cha kigaidi ambacho kilitekelezwa na jeshi la kigeni linalopatikana kwenye ardhi ya Congo.

===
At least 11 people were killed and scores injured Thursday when explosions in the eastern Congo city of Bukavu struck a rally held by leaders of the M23 rebel group, which took control of the city earlier this month.

Rebel leaders blamed the bombing on Congo’s government and said attackers were among those killed in the blasts, with conflicting reports among rebels and local officials about the number of attackers and victims. Congo’s president blamed the attack on unspecified “foreign” forces.

“The attack caused 11 deaths and verifications are underway. The author of the attack is among the victims,” Corneille Nangaa, leader of the Congo River Alliance (AFC), which includes the M23, told reporters. “There are 65 injured, six of whom are seriously injured and are currently being treated in the operating room.”

He said that “following today’s unfortunate incident, we are obliged to react.”

Leaders of the M23 rebel group, including Nangaa, were meeting residents when the explosions occurred in the central part of Bukavu. Video and photos shared on social media showed a crowd fleeing the mass rally in Bukavu and bloodied bodies on the ground.

Source: AP News
 
Wakongoman Wana Matatizo sehemu....!
Kwa kile M23 inachofanya Congo, Tena kesho mkajazane kwenye Mkutano wao...!
 
Nikajua kujitoa mhanga ni kwa magaidi tu! Tuombe sana hii culture wabaki nayo magaidi isienee kwa jamii zingine.
 
M23 inatengeneza uongo ili ipate uungwaji mkono na jumuiya za kimataifa
 
Back
Top Bottom