Watu 12 wafariki DR Congo kutokana na mgodi uliovuja sumu Angola

Watu 12 wafariki DR Congo kutokana na mgodi uliovuja sumu Angola

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289


Karibu watu 4,500 wameugua kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia kuvuja kwa sumu kutoka kwa mgodi wa almasi katika nchi jirani ya Angola, waziri wa mazingira anasema.



Eve Bazaiba alisema watu 12 walikuwa wamefariki dunia. Alisema kuwa DR Congo itauliza fidia ya uharibifu uliosababishwa lakini haikutaja kiasi.

Hata hivyo, hadi kufikia hivi sasa hakuna aliyesema chochote kujibu hayo hasa kutoka kwa kampuni ya madini.

Mwezi uliopita kulikuwa na uvujaji wa kutoka eneo la uhifadhi wa bidhaa za vyuma vizito uliosababisha mto kuwa na rangi nyekundu, samaki, viboko na wanyama wengine wakafa.
 
Wapumzike kwa amani wapambanaji
Waliokufa sio wafanyakazi wa mgodi ila ni raia wa kawaida wasiohusiana kabisa na huo mgodi...
Watu wa mgodi wamepollute maji ya mto kwa sumu zao, maji ambayo yanatumika na wanajamii wengine kwa matumizi yao ya kawaida ikawapelekea kupata madhara ikiwemo kuugua na wengine kufariki dunia
 
Back
Top Bottom