John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Watu 13 akiwemo mtoto mmoja wamefariki dunia baada ya kuangukia ndani ya kisima wakati wa sherehe ya harusi Kaskazini mwa India, juzi Februari 16, 2022.
Waliopoteza maisha asilimia kubwa ni wanawake na mtoto huyo ambapo walikuwa wamekaa juu ya kisima kilichokuwa kimezibwa kwa muda.
Taarifa ya Polisi wa Jimbo la Kushinagar ambapo ndipo tukio lilipotokea wamekiri kutokea kwa maafa hayo huku mmoja akijeruhiwa.
"Tukio hili limetokea wakati wa sherehe za ndoa, upelelezi unaendelea,” amesema Polisi wa Kushinagar, Sachindra Patel.
Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi amelitaja tukio hilo kuwa ‘linaloumiza moyo’.
Waziri Modi ametangaza kutoa fidia ya dola 2,662 kwa kila familia iliyokumbwa na majanga hayo, pia dola 665 kwa kila familia ambayo imepata majeruhi katika tukio hilo.
Mamlaka ya Wilaya ya Kushnigar nayo imeongeza kwa kutoa dola 5,323 kwa kila familia iliyoathirika na tukio hilo.