#COVID19 Watu 15 wafariki huku 24 wakilazwa hospitali sababu ya Corona Zanzibar

#COVID19 Watu 15 wafariki huku 24 wakilazwa hospitali sababu ya Corona Zanzibar

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Watu 15 wamefariki na wengine 24 wamelazwa hospitali wakiendelea kupata matibabu kutokana na virusi vya ugonjwa wa Corona Zanzibar.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya wa Zanzibar Mhe Nassor Ahmed Mazrui wakati akitoa takwimu za ugonjwa wa Corona kuanzia Juni 25 hadi Agosti 10.

Waziri Mazrui amesema jumla ya watu 29,326 wamepimwa virusi vya Corona na 390 wamekutwa na virusi hivyo huku wageni wakiwa ndio wengi 278.

Akizungumzia chanjo ya Corona Mhe Mazrui amesema Zanzibar ina chanjo za aina mbili Sinovac ya china na Sputnik light 5 na chanjo hizo zimeanza kwa makundi.
 
Nyie endeleeni tu na zoezi lenu la chanjo zenu basi hizi takwimu za mafungu mafungu hazina msaada wowote.
 
Back
Top Bottom