Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Raia 18 nchini Niger wameuawa katika shambulio la wanamgambo magharibi mwa nchi hiyo, serikali inasema.
Majambazi waliokuwa na pikipiki walivamia lori lililokuwa likisafirisha watu kati ya vijiji viwili vya mkoa wa Tillaberi.
Magharibi mwa Niger - kama vile nchi jirani za Mali na Burkina Faso - kwa miaka mingi imekuwa ikikabiliwa na mashambulio ya wanamgambo, licha ya juhudi za vikosi vya kimataifa vilivyotumwa katika eneo la Sahel kupambana na wanamgambo wa kijihadi.
Majirani wote wawili wa Niger sasa wana serikali za kijeshi baada ya wakuu wa jeshi kuwatimua tawala za kiraia, wakisema wameshindwa kukabiliana na uasi.