Watu 19 waliokimbia majumbani mwao kwenda kupanga Wataweza kuishi huru na baba mwenye nyumba?

Watu 19 waliokimbia majumbani mwao kwenda kupanga Wataweza kuishi huru na baba mwenye nyumba?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Binadamu aliyekamilika anahitaji amani ya nafsi ili aweze kusherekea matumizi mazuri ya kipato alichonacho.

Upo Uhuru mkubwa unapoishi kwako kuliko unapokuwa nyumba za kupanga hasa hizi ambazo mwenye nyumba ni mtu mweusi mwenye ila na wivu juu ya mafanikio yako.

Hakuna binadamu mwenye akili timamu anayekubali kupoteza amani ya nafsi anayopata nyumbani kwake na kukimbilia kero na karaa za baba mwenye nyumba akiwa mpangaji.

Karaha za baba mwenye nyumba uanzia anavyokupokea. Ukiona baba mwenye nyumba akukaribishi ndani mnasaini mkataba ukiwa nje au gereji Basi tambua ukikabidhiwa funguo utaishi apendavyo siyo upendavyo.

Katika hatua za awali atawalazimisha mbwa wasikubwekee na ikiwezekana atalazimika kuwafunga kamba wasikubughudhi ili uone upo salama.

Siku watoto wake watakapotoka shule nakumweleza kwamba mpangaji flani ni mkorofi, ataki kusikiliza au anataka kuwatawala Basi ndipo utagundua ubaya wa baba mwenye nyumba.

Anaweza kupa kila unachohitaji na wakati mwingine atakupa gari yakutembelea ila tegemea kuulizwa utarudi saa ngapi, mbona mafuta yameisha, kwanini umempa jirani yetu lifti kwenye gari wakati atusalimiani, kwanini unachati na marafiki zako wa zamani wakati uliniambia mmegombana, kwanini unajidai kujua sana kujadili na kwanini kila tukiongea unaonekana unakosoa namna nilivyojenga nyumba yangu nk jiandae kwa haya.

Hakuna Mwanadamu aliyewahi kuhama nyumbani kwake akaenda kupanga jirani anayekuwa na amani. Kila saa utatamani kurudi kusalimilia japo majirani lakini watakushangaa. Siku utakapotaka kurejea yawezekana ukakuta tayari ndani Kuna nyoka na wadudu wengine wengi, utakuta kiti chako anakalia mwingine omba usikute kakalia kichaa aliyechoka kurandaranda mtaani.

Niwaombe tufahamu kwamba wenzetu wamekwenda kupanga, hata mwezi bado tayari wanaomba kurejea kwenye nyumba zao bila kufahamu kwamba wakati wanaondoka waliwatukana majirani na Kuna kesi yakufukuzwa kwenye mtaa ilifanyika na wakaazimia kumfukuza. Ni vigumu kumwomba mjumbe msamaha wanakijiji wakakuelewa maana wao ndio uliowakose siyo mjumbe. Unaanzaje kuwaomba wanakijiji msamaha?
 
Back
Top Bottom