joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Mafisa nchini Kenya wamethibitisha kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana n atukio la maporomoko ya udongo katika eneo la Pokot magharibi imefikia 37 .
Hii ni baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko iliyotokana na mvua kubwa inayonyesha katika eneo hilo.
Maporomoko hayo yalioathiri zaidi vijiji vya Nyarkulian na Parua, yameripotiwa kusababishwa na mvua kubwa inayoripotiwa kuendelea kunyesha katika eneo hilo.
Vijiji hivyo vinasemekana kutenganishwa kabisa na mafuriko ambayo yameharibu daraja.
Maafisa pia wamesema kuwa miili ya watu 12, ikiwemo ya watoto saba zilipatikana asubuhi ya Jumamosi.
Joel Bulal, mmoja wa wasimamizi wa serikali katika eneo hilo ameliambia gazeti la Daily Nation kuwa shughuli za uokozi zinaenedelea huku na kuwatafuta wale ambao hawajulikani waliko
Kamishena wa jimbo hilo Apollo Okelo amesema watu wengine wengi huenda wamekwama chini ya matope na kuongeza kuwa shughuli ya kuwaokoa zinaathiriwana hali mbaya ya hewa.
"Tunajaribu kutafuta mahali ambapo daraja limesombwa na maji ya mafuriko,"alinukuliwa na mtando wa habari wa Standard nchiniKenya.
Picha zinazosambazwakatika mitandao ya kijamii zinaonesha miti iliyosombw ana maji na mingine kung'olewa, huku matope yakisambaa barabrani
Katika Twitter yake, Shirika la Msalaba mwekundu limethibitisha ripoti zinazoashiria tukio la maporomoko "makubwa" ya matope.
Kumeshuhudiwa mvua nyingi katika eneo la Afrika Mashariki na upembe wa Afrika kwa wiki kadhaa sasa.
Kijiji kizima kimesombwa na maji nchi Sudan Kusini huku visa ajaliya maporomoko ya ardhi ikiripotiwa Tanzania, Ethiopia na Somalia.
Wanasayansi wanasema hali mbaya ya hewa inatarajiwa kukumba baadhi ya nchi katika kanda hiyo kwasababu viwango vya joto katika bahari Hindi vinatarajiwa kupanda kupita kiasi cha kawaida, hali ambayo huenda ikasababisha mvua kubwa .