Watu 4 wafariki kwenye ajali wakitokea msibani

Watu 4 wafariki kwenye ajali wakitokea msibani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Jumla ya watu sita walikuwa kwenye gari hilo na walikuwa njiani kurejea Nairobi baada ya kuhudhuria mazishi Eneobunge la Kiharu

- Dereva alipopoteza mwelekeo wa gari hilo na kuyumba nje ya barabarani kabla ya kugonga miti na kuingia kwenye bonde
- Akithibitisha tukio hilo jioni, Kamanda wa Polisi Kaunti ya Murang’a Josphat Kinyua alisema wanne kati ya watu hao walifariki dunia mara baada ya ajali hiyo kutokea


Watu wanne wameangamia na wawili kujeruhiwa vibaya kwenye ajali iliyotokea Jumanne, Agosti 6, katika eneo la Ithe Ruui kwenye Barabara ya Kenol-Murang’a.

Sita hao walikuwa njiani kurejea Nairobi baada ya kuhudhuria mazishi Eneobunge la Kiharu, wakati dereva alipopoteza mwelekeo wa gari hilo na kuyumba nje ya barabarani kabla ya kugonga miti na kuingia kwenye bonde.
Watu 4 waangamia kwenye ajali baada ya kuhudhuria mazishi Murang'a

Gari aina ya Toyota Wish lililohusika katika ajali eneo la Ithe Ruui kwenye Barabara kuu ya Kenol-Murang'a mnamo Agosti 6, 2019.

Akithibitisha tukio hilo jioni, Kamanda wa Polisi Kaunti ya Murang’a Josphat Kinyua alisema wanne kati ya watu hao walifariki dunia mara baada ya ajali hiyo kutokea.

Kwa mujibu wa Citizen Digital, wawili walionusurika walipelekwa katika Hospitali ya Maragwa wakiwa na majeraha mabaya.

Ingawa chanzo cha ajali hiyo hakikujulikana mapema, wakazi katika eneo hilo waisema kwamba, eneo hilo linafahamika sana kwa ajali nyingi kaunti hiyo.
Miezi miwili iliyopita, naibu chifu wa Nginda aliripotiwa kuaga dunia kufuatia ajali ya barabarani eneo hilo.

Pia Waziri wa Maji wa Kaunti Water Paul Macharia, alihusika katika ajali ambayo ilimuua dereva wake kwenye barabara hiyo.
Source: Tuko
 
Back
Top Bottom