Watu 5 wamefariki dunia ndani ya siku 7 katika matukio tofauti mkoani Ruvuma

Watu 5 wamefariki dunia ndani ya siku 7 katika matukio tofauti mkoani Ruvuma

Tengosmileog

New Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
1
Reaction score
0
Watu watano wamepoteza maisha mkoanii Ruvuma kwa muda wa siku 7 likiwemo la mwanafunzi a kidato cha kwanza Sekondari ya Mbinga wilayani na mtumbo la kucharazwa viboko hadi kufa. Kamanda wa Polisi Ruvuma Bw Joseph Konyo anawashikilia walimu 6 katika tukio hilo ambalo hakuwataja majina kwa ajili ya uchunguzi.

Pia kamanda Konyo amesema Mtu asiyejulikana alimgongea mzee mmoja uko kijiji cha Marungu wilayani Nyasa na kumshusha kitandani mpaka chini na kumkata na shokaa na kusababisha kifo chake.

Taarifa nyingi ni kutoka wilayani Mbinga ambako kijana mmoja ameuawa na kukatwa miguu kwa tuhuma za wizi wa kuku.

=====

Mwanafunzi afariki baada kucharazwa bakora na mwalimu Ruvuma.

Watu 5 wamefariki dunia ndani ya siku 7 katika matukio tofauti mkoani Ruvuma likiwemo la mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Shule ya sekondari Mbinga wilayani Namtumbo kufariki dunia baada ya kupigwa viboko na walimu wake.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Joseph Konyo amesema wanawashikilia walimu sita kutokana na kifo cha mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 15 ambaye hajamtaja jina kwa sababu za uchunguzi.

Katika matukio mengine Kamanda Konyo amesema mzee wa miaka 85 mkazi wa Kijiji cha Marungu Wilayani Nyasa aligongewa mlango na alipofungua mtu asiyefahamika aliingia ndani na kumvuta chini kutoka kitandani na kumkata kwa shoka na katika tukio lingine la mauaji limetokea Wilayani Mbinga, ambapo mtu mmoja ameuawa kwa kukatwa miguu kwa tuhuma za wizi wa kuku.

Chanzo: ITV
 
MWANAFUNZI wa Shule ya Sekondari wilayani Namtumbo, Mkoa wa Ruvuma mwenye umri wa miaka 15 (jina limehifadhiwa), amefariki dunia kwa madai ya kupewa adhabu ya kipigo na walimu wake baada ya kufanya vibaya mitihani ya Mock mkoa.

Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma, Joseph Konyo, akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, alisema katika tukio la kwanza Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi wa kifo cha mwanafunzi huyo ambaye inadaiwa Julai 18, mwaka huu majira ya saa 3:00 asubuhi katika kituo cha Polisi cha Namtumbo kilipokea taarifa za kifo chake.

Alisema inadaiwa katika taarifa hiyo mwanafunzi huyo alifariki wakati akipatiwa matibabu Kituo cha Afya cha Hanga baada ya kulazwa kutokana na majeraha ya kupewa adhabu ya kuchapwa viboko yeye pamoja na wanafunzi wenzake wa kidato cha kwanza na cha tatu.

Alisema inadaiwa Julai 19, mwaka huu, majira ya saa 5:00 asubuhi mwanafunzi huyo akiwa na wenzake walipewa adhabu na walimu wao kwa kufanya vibaya kwenye matokeo ya Mock mkoa walioufanya kabla ya kufungwa shule.

Alisema inadaiwa baada ya adhabu hiyo mwanafunzi huyo aliumia na kupata uvimbe kwenye paja la upande wa kulia pia katikati ya mgongo na ndipo wazazi wake walipompeleka Kituo cha Afya Hanga na siku ya pili majira ya saa 10:00 jioni mwanafunzi huyo alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu.

Kamanda Konyo alisema, walimu sita wa Shule ya Sekondari Mbunga wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.

Alilitaja tukio lingine la Julai 17, mwaka huu majira ya saa 7:00 mchana katika Kijiji cha Marungu, Kata ya Tingi, wilayani Nyasa, mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 85 (jina limehifadhiwa) mkazi wa Kijiji cha Marungu aliuawa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake kisha kukatwa na shoka kichwani na mtu asiye fahamika.

Inadaiwa kabla ya tukio hilo mwanaume huyo alikuwa amelala nyumbani kwake na mkewe mwenye umri wa miaka 84.

Kamanda alisema, alikuja mtu na kuanza kugonga mlango kwa nguvu kama anabisha hodi bila kusema chochote ndipo mwanaume huyo alipolazimika kuamka na alipofungua mlango alivutwa nyuma ya nyumba yake na kuangushwa china kisha mtuhumiwa akaingia ndani na kuchukua shoka lililokuwa sebuleni ambalo alilitumia kumkata kichwani na kumsababishia kifo mzee huyo ambaye inadaiwa alikuwa akilalamikiwa kwa imani za kishirikiana. Polisi inaendelea kumsaka mtuhumiwa wa tukio hilo.

Katika tukio la tatu inadaiwa Julai 17, mwaka huu, majira ya saa 4:00 usiku katika Kijiji cha Lugali, Kata ya Mkumbi, wilayani Mbinga, mwanaume mwenye umri wa miaka 40 mkazi wa Kijiji cha Ngima wilayani humo, aliuawa na watu waliojichukulia sheria mkononi kwa kumkata miguu na mwili kwa kutumia kitu chenye ncha kali wakimtuhumu kuwa ni mwizi wa kuku.

Katika tukio hilo polisi inamshikilia mtuhumiwa mmoja na msako wa kuwakamata wahusika wengine unaendelea.

Pia, katika tukio lingine Julai 18, mwaka huu majira ya saa 2:00 usiku katika Kijiji cha Mtumbati Maji, Kata ya Mgombasi, mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 25, mkazi wa kijiji hicho alikutwa akiwa amefariki kwenye tembe la kuchomea tumbaku.

Alifafanua zaidi kuwa inadaiwa mwanaume huyo alikuwa ameenda shambani Julai 17, mwaka huu, kukagua maendeleo ya uunguaji wa tumbaku yake na alikuwa anaichoma na ndipo alipopatwa na ajali ya kuangukia kwenye shimo la tumbaku na kufia humo baada ya kuvuta hewa ya ukaa (carbon monoxide).

Kamanda Konyo alitoa rai kwa wananchi wanaojichukulia sheria mkononi kuacha mara moja.

Ippmedia
 
Aisee babu miaka 85 Bibi miaka 84 inatosha ,nyinyi walimu mishahara mwaka wa kumi huu hamjaongezewa hamu ya kuchapa inatoka wapi? Pale kwa mwizi sina cha kuongeza apigwe tu
 
Watu watano wamepoteza maisha mkoanii Ruvuma kwa muda wa siku 7 likiwemo la mwanafunzi a kidato cha kwanza Sekondari ya Mbinga wilayani na mtumbo la kucharazwa viboko hadi kufa. Kamanda wa Polisi Ruvuma Bw Joseph Konyo anawashikilia walimu 6 katika tukio hilo ambalo hakuwataja majina kwa ajili ya uchunguzi.

Pia kamanda Konyo amesema Mtu asiyejulikana alimgongea mzee mmoja uko kijiji cha Marungu wilayani Nyasa na kumshusha kitandani mpaka chini na kumkata na shokaa na kusababisha kifo chake.

Taarifa nyingi ni kutoka wilayani Mbinga ambako kijana mmoja ameuawa na kukatwa miguu kwa tuhuma za wizi wa kuku.

=====

Mwanafunzi afariki baada kucharazwa bakora na mwalimu Ruvuma.

Watu 5 wamefariki dunia ndani ya siku 7 katika matukio tofauti mkoani Ruvuma likiwemo la mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Shule ya sekondari Mbinga wilayani Namtumbo kufariki dunia baada ya kupigwa viboko na walimu wake.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Joseph Konyo amesema wanawashikilia walimu sita kutokana na kifo cha mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 15 ambaye hajamtaja jina kwa sababu za uchunguzi.

Katika matukio mengine Kamanda Konyo amesema mzee wa miaka 85 mkazi wa Kijiji cha Marungu Wilayani Nyasa aligongewa mlango na alipofungua mtu asiyefahamika aliingia ndani na kumvuta chini kutoka kitandani na kumkata kwa shoka na katika tukio lingine la mauaji limetokea Wilayani Mbinga, ambapo mtu mmoja ameuawa kwa kukatwa miguu kwa tuhuma za wizi wa kuku.

Chanzo: ITV
Heading watu watano, content wanatajwa watu watatu
 
Haya mambo ya kishenzi ya jamii zisizostaarabika ya kupiga watoto yafike mwisho sasa.
 
Adhabu ya viboko kwa watoto ni ukatili uliopaswa kubaki karne ya 19.
 
Back
Top Bottom