Watu 6 zaidi wafungua kesi ya Unyanyasaji dhidi ya Lizzo

Watu 6 zaidi wafungua kesi ya Unyanyasaji dhidi ya Lizzo

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Madai Mapya ya Unyanyasaji wa 'Dancers' yaibuliwa dhidi ya Mwanamuziki Lizzo, (Melissa Viviane Jefferson) baada ya Watu 3 kufungua madai kama hayo Wiki iliyopita

Mawakili wanaowakilisha Wacheza Dansi Watatu wa zamani wa Lizzo wamesema wanachunguza malalamiko mapya yaliyotolewa na watu 6 zaidi ambao walifanya kazi na Mwimbaji huyo

Watu hao wanatajwa kuwa walishiriki katika kuandaa 'Reality Show' ya Lizzo katika Studio za Amazon iitwayo "Lizzo's Watch Out for the Big Grrrls."

Mwanasheria wa Masuala ya Ajira, Ron Zambrano, amesema madai hayo yanahusu "mazingira yenye kashfa ya kingono" na kutofuatwa kwa malipo ya Wafanyakazi

Agosti 1, 2023 Wacheza Dansi Watatu waliofanya ziara ya Muziki na Lizzo, (Arianna Davis, Noelle Rodriguez na Crystal Williams) walifungua kesi wakidai walinyanyaswa Kingono, Kidini, Kwa misingi ya Rangi, na kufungwa kwa Sababu za Uongo na Mwanamuziki huyo

Akizungumzia tuhuma hizo, Lizzo amedai Madai yaliyotolewa dhidi yake siyo ya kweli na kuwa yeye sio muovu kama Vyombo vya Habari vinavyomwonesha


Chanzo: BBC
 
Back
Top Bottom