Watu 60 wafariki katika mlipuko wa mgodi wa dhahabu Burkina Faso

Watu 60 wafariki katika mlipuko wa mgodi wa dhahabu Burkina Faso

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
1645532410605.png

Takriban watu 60 waliuawa siku ya Jumatatu katika mlipuko katika mgodi wa dhahabu katika kijiji karibu na Gaoua kusini-magharibi mwa Burkina Faso.

Makumi ya watu zaidi walijeruhiwa, wakiwemo wanawake na watoto

Ilitokea wakati vilipuzi vilivyohifadhiwa karibu na eneo la kuchimba dhahabu vilipolipuka, maafisa wa eneo hilo na mashahidi walisema.

Wengi wa watu waliojeruhiwa walihamishwa hadi hospitali ya mkoa ya Gaoua.

Mwendesha mashtaka wa mkoa aliyetembelea eneo la tukio alisema uchunguzi umeanzishwa kuhusu mkasa huo.

Ajali hutokea mara kwa mara katika shughuli za uchimbaji madini ambazo hazijaidhinishwa katika baadhi ya nchi za Afrika, huku udhibiti wa usalama mara nyingi ukiwa mdogo au haupo kabisa.

BBC Swahili
 
Inakuwaje baruti na vifaa like pin zitunzwe eneo karibia na mgodi? Hapo vilipuzi vinakuwa kama trigger tu yakupolomosha ardhi ambayo ndiyo huleta madhara makubwa kwa wachimbaji na watu wote waliopo eneo husika.

Kidogo Tanzania kusikia vilipuzi vimeripuka ni mara chache tofauti na majanga ya maji kuingia migodini au maji kulegeza ardhi na kuporomoka.

High level of precaution is needed
 
Back
Top Bottom