Watu 7 wakamatwa nchini Uganda kwa kupinga kikomo cha umri wa mtu anayegombea rais

Watu 7 wakamatwa nchini Uganda kwa kupinga kikomo cha umri wa mtu anayegombea rais

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
Takriban watu saba wametiwa nguvuni katika mji mkuu wa Uganda Kampala, kufuatia maandamano ya kupinga mapendekezo ya muswada wa sheria unaoondoa kikomo cha umri wa mtu anayegombea urais.

Katiba ya sasa inasema kikomo cha umri wa urais ni miaka 75.

Mabadiliko ya katiba yatamruhusu rais Yoweri Museveni kugombea tena urais mwaka 2021.

Umri halisi wa rais Museveni haufahamiki, lakini mtandao wa Wikipedia unasema ana umri wa miaka 73

Wanaharakati vijana wa kundi lijulikanalo kama 'The Alternative', ambao waliandaa maandamano hayo, wanasema ofisi yao ilivamiwa jana na wanajeshi pamoja na polisi.

Wanadai laptop, compyuta pamoja na nyaraka nyingine za kampeni yao vilichukuliwa wakati wa uvamizi huo.

CHANZO: BBC
 
Sasa huyu anatofauti gani na yule anayekataza watu wasimwombee mgonjwa?
 
Huyo Dikteta ndio anamuambukiza na Mkulu wetu aisee.
 
Hapa kwetu napo tujiandae kukamatwa tutakapopinga mtakatifu asifanye uchaguzi
 
Back
Top Bottom