Watu 7 wauawa Kashmir katika mapigano kati ya India na Pakistan

Watu 7 wauawa Kashmir katika mapigano kati ya India na Pakistan

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Maafisa wa kijeshi nchini India wamesema makabiliano kati ya wanajeshi wa Pakistan na India katika eneo lililo na utata la Kashmir yamesababisha mauaji ya watu 7 kutoka pande zote mbili.

Jeshi la India limesema wanajeshi wa Pakistan mapema hii leo walilenga eneo moja la mpaka wake na eneo lililo na watu wengi mjini Kashmir na kusababisha muaji ya wanajeshi wawili pamoja na raia mmoja.

Msemaji wa jeshi la India Kanali Rajesh Kalia, amesema raia wengine watatu wa India waliuwawa kupitia shambulizi lililofanywa na Pakistan.

Kanali Kalia ameyaita mashambulizi hayo kama hujuma isiyozuilika inayokiuka makubaliano ya kusitisha mapigano ya mwaka 2003 kati ya India na Pakistan.

Pakistan kwa upande wake imesema wanajeshi wa India wamewaua raia watatu na mwanajeshi mmoja na kuwajeruhi raia watano na wanajeshi wawili katika mpaka unaoigawa Kashmir kati ya mataifa hayo mawili hasimu.

India na Pakistan zimekuwa zikikwaruzana kwa muda mrefu kutokana
 
Filamu nyingi za India zinazungumzia hii kitu na athari zake ukipata muda check " GADAR EK PREM KATHA -2001 ( Sunny deol, Amrish puri, Amisha patel)
images%20(4).jpeg
 
Back
Top Bottom