Watu 72 wamepoteza maisha nchini Afrika Kusini kufuatia ghasia zinazoendelea

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Watu 72 wamepoteza maisha nchini Afrika Kusini kufuatia ghasia zinazoendelea kushuhudiwa kati ya wafuasi wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Jacob Zuma na maafisa wa usalama.

Kwa siku zipatazo tano, wafuasi wa Zuma ambaye anaendelea kutumikia kifungo chake cha miezi 15 jela, wamekuwa wakiandamana katika miji mbalimbali nchini Afrika Kusini kushinikiza kuachiliwa huru kwa kiongozi wao. Machafuko hayo yanakwenda sambaba na waandamanaji kufanya vurugu kwa kuvunja na kuvamia maduka makubwa nchini humo katika jiji la Johannesburg na mkoa wa KwaZulu-Natal.

Licha ya Rais Cyril Ramaphosa kuagiza kutumwa kwa wanajeshi zaidi ya Elfu mbili kuzuia wizi wa mali na maandamano hayo, hali inaoenekana kuendelea kuwa mbaya. Maafisa wachache wa usalama wameoneakana karibu na maduka yanayoporowa na wananchi wa taifa hilo, huku idadi ya vifo ikiendelea kupanda,hasa kutokana na watu kukanyagana.

Watu wengine zaidi ya Elfu Moja na mia mbili wamekamatwa katika machafuko hayo. Wafuasi wa Jacob Zuma wanasema wataendelea kuandamana hadi kiongozi wao atakapochiliwa huru.

Bongo5
 
Hawa watu wa SA tokea walivyofanya ile kuwa katakata waafrica wenzao kipindi kile sija wahi tena kuwapenda including their art works and any product from SA. Wacha wauwane wezi wote hao

Huo uporaji una husiana na nini na anayetumikia kifungo chake kisheria.
 
Ma Sauzi mapumbavu kweli
 
Wezi tu hao. Sijawahi ona watu makatili na roho mbaya kama hao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…