Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Polisi nchini Uganda inawashikilia wahudumu wawili wa afya kwa madai ya kuhusika kuwachoma takriban watu 800 chanjo feki za corona mwezi uliopita.
Mtu mmoja, ambaye ni daktari, anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika kuwachoma watu hao chanjo katika mji wa Kampala kati ya Mei 15 na Juni 17, huku baadhi ya waliochomwa chanjo hiyo wakiripotiwa kufariki katika wimbi la pili la corona.
Polisi wamewatoa hofu wananchi kuwa chanjo hizo zinaweza kuwa ni maji tu yaliyowekwa katika chupa zilizofanana na chupa halisi za chanjo ya corona. Waliochomwa chanjo hiyo walilazimika kulipa kati ya Shilingi za Uganda 100,000 na 200,000 (sawa na Shilingi 65,000 na 130,000 za Tanzania).
Operesheni ya polisi iliyofanyika June 17 ilifanikiwa kuwakamata manesi wawili pamoja na kitabu kilichokuwa na majina ya wote waliochomwa chanjo hiyo pamoja na namba za utambulisho baada ya kuchoma chanjo hiyo.
Manesi hao walikutwa pia na mihuri ya Mamlaka za Jiji la Kampala na Kituo cha Afya cha Kiswa, pamoja na dozi 90 za chanjo hiyo feki, pamba na glovu, na walikuwa na vitambulisho vya Mamlaka za Jiji, ambapo baada ya kuulizwa, Mamlaka zilikana kuwafahamu watu hao kuwa waajiriwa wake.
Chanzo: Daily Monitor