Ule msemo wa 'people get the president they deserve' (watu hupata rais aliye stahili yao) una ujumbe muhimu katika MMU. Kama una mpenzi ujue yeye ndiye stahili yako. Hivyo, acha kudai eti oh huna bahati ya kuwa na mtu mzuri maishani. Hukulazimishwa kuwa naye. Na hulazimishwi kuendelea kuwa naye tu. Daima uamuzi ni wako. Tulia. Tafakari. Chukua hatua. Usihofu. Fanya maamuzi magumu. Ndio. Leo leo. Usisubiri kesho maana kesho haiji.
Not always. . .
Unalosema lingekuwa kweli tu iwapo kila mtu angekua anamjua mwenzie kwa kila namna kabla ya kumkubalia/kumuomba mahusiano.
mie ananiudhi ila simwachi.
Lizzy, huwezi kumjua mtu 100%, true that. Ila kuna mtu anaanzisha mapenzi na mwenzie wakati hata hawajafahamiana vya kutosha, halafu wanalalamika kua mpenzi wangu hayupo nilivo tarajia. Imagine watu wanakutana facebook na kuanzisha mapenzi hata kabla ya kuonana. Hapo akikuta mtu ni mbovu, si atakua amejitafutia? na atakua amestahili chochote kitakacho tokea?Not always. . .
Unalosema lingekuwa kweli tu iwapo kila mtu angekua anamjua mwenzie kwa kila namna kabla ya kumkubalia/kumuomba mahusiano.
Hiyo ni kwa sababu muda wa kumtafuta mtu stahiki umeshapita!Compa are you in L.O.V.E ??? Umempata anayestahili eeh!
Upande wangu, nimempata mwenyewe..tunastahiliana🙂)
Ndo hapo sasa. . .Lizzy, huwezi kumjua mtu 100%, true that. Ila kuna mtu anaanzisha mapenzi na mwenzie wakati hata hawajafahamiana vya kutosha, halafu wanalalamika kua mpenzi wangu hayupo nilivo tarajia. Imagine watu wanakutana facebook na kuanzisha mapenzi hata kabla ya kuonana. Hapo akikuta mtu ni mbovu, si atakua amejitafutia? na atakua amestahili chochote kitakacho tokea?
wewe mkuu wangu unataka kuvunja ndoa za watu