Watu kama Ahmed Ally huja mara moja katika maisha yetu

Watu kama Ahmed Ally huja mara moja katika maisha yetu

ninosi

Senior Member
Joined
Jun 30, 2022
Posts
151
Reaction score
333
Watu kama Ahmed Ally ambae ni Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC huja mara moja katika maisha (once in a life time).

Kutokana na uwezo mkubwa alionao Ahmed amekua akifanya kazi za taaluma mbalimbali na kwa ufanisi mkubwa sana. Mfano:-

1. Afisa Habari
Ukiwa unamsikiliza Ahmed anatoa taarifa kuhusu timu yake huchoki kumsikiliza. Saa nyingine huwa nawaza kwanini Ahmed usianzishe darasa, ili kina Kamwe na wenzake waje wajifunze kwako?!

2. Digital Manager
Ukiangalia jinsi akaunti za Simba SC zinavyoendeshwa, ni very professional. Hii imefanya Simba SC kuwa moja ya vilabu bora duniani vinavyofatiliwa sana mitandaoni. Priva na wenzako mnalakujifunza hapa.

3. Afisa Muhamasishaji
Kuna kipindi timu fulani iliunda kikundi cha watu ili kuhamasisha mashabiki wake waende katika tamasha lao lakini wapi. Kwa Simba SC hali ilikua tofauti kabisa. Ahmed alishika kispika tu, Taifa ikajaa hadi pomoni. Hii haikuja bure, bali ni kutokana na elimu bora kabisa (Public Relationship and Advertising) aliyoipata chuo kikuu cha dar es salaam.

4. MC. Ahmed ni full package linapokuja swala la shughuli ya 'Msema Chochote'. Hili alilidhihirisha siku ya Simba Day tofauti na wale jamaa ambao iliwabidi wakodi ma MC wa sherehe za mitaani ili tamasha lao lifane, lakini wapi.

USHAURI WANGU KWA SIMBA SC:
Ahmed anapoelekea kutimiza mwaka mmoja Wa kuitumikia Simba SC (3/1/2023), viongozi:-

1. Mumuongezee Ulinzi. Kwa anavyowacharura Uto ambao wametoka kutandikwa 'Ndoige', usalama wake unahitaji kuimalishwa zaidi.

2. Mumuongezee Shekeli. Japokuwa Simba SC ndo timu inayolipa vizuri zaidi, ila Ahmed aangaliwe kwa jicho la tofauti. Nasema hivi kwasababu kuna timu imebidi iajiri vijana watatu ili wafanye kazi ambazo Ahmed huzifanya peke yake. Ni bahati iliyoje kua na Ahmed Ally.

MWISHO:
Aliyemleta Ahmed Ally (a.k.a Semaji la Kimataifa), Simba SC, peponi moja kwa moja.

maxresdefault.jpg
 
Ukisikia zezeta ndo huyu jamaa anamwabudu binadamu mwenzake wakati muumba wake hajawahi kumshukuru na kumsifu hata kwa sekunde.
 
Anafanya kazi nzur ila co kwa sifa zote hizo,halafu pepo co jambo jepesi kama unavyojiaminisha
 
Huu sasa ndio upuuzi wa Karne, yaani mtu unaamzisha Uzi wa kujisifu na kujitukuza mwenyewe!! Wewe Subiri mdawako ukifika huitaji kujisifia wadau wataiona kazi Yako [emoji1][emoji1][emoji1]. Kila Jambo linawakati wake.
 
Peponi moja kwa moja???
Mwambie afanye ibada.
Mkuu hiyo in lugha ya picha.
Anafanya kazi nzur ila co kwa sifa zote hizo,halafu pepo co jambo jepesi kama unavyojiaminisha
Wapi nimempa sifabadizostahili? Ahmed Ally ni full package. Kuhusu pepo no lugha ya picha uliyotumika, ni kimaamisha aliyemleta anahitaji kupatiwa zawadi yenye thamani kubwa sana.
 
Ukisikia zezeta ndo huyu jamaa anamwabudu binadamu mwenzake wakati muumba wake hajawahi kumshukuru na kumsifu hata kwa sekunde.
Mkuu wapi nimeliabudu Semaji la Kimataifa? Vipi lakini umepata chai kweli, mana naona 'dishi' lako kama halipo sana? Karibu mihogo nipo kwa Ashura Cheupe hapa.
mihogo-karai-recipe-main-photo.jpg
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Mlete Mzungu..

Huyu jamaa hata kwenye Hamasa hajambo.

Nilimpenda sana kwenye nyinbo ya Hawaamini macho Yao.

BONGE LA songi Hawaamini macho Yao.....
 
Mlete Mzungu..

Huyu jamaa hata kwenye Hamasa hajambo.

Nilimpenda sana kwenye nyinbo ya Hawaamini macho Yao.

BONGE LA songi Hawaamini macho Yao.....
Kabisa Mkuu... Kuna jamaa walijaribu kuiga wakafanya hadi rehearsal siku ya mechi baada ya kupelekewa pumzi ya moto wakapoteana.
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Siku hizi kwenye mpira wa kibongo, wasemaji wa timu ni maarufu kuliko hata wachezaji
 
Back
Top Bottom