DHANA YA UMAARUFU
Jamii ni mkusanyiko wa watu wenye hali na mitazamo tofauti wakiwa chini ya mamlaka moja ambapo kila mmoja ana mchango kwa maisha ya mwingine.
Katika jamii zilizoendelea, hali ya kutegemeana ni kubwa kutokana na kila mwanajamii kuwa na shughuli halali inayoathiri maisha ya wengine.
Hata hivyo, wapo ambao shughuli zao hugusa maisha ya walio wengi zaidi kuliko wengine. Kutokana na kugusa hisia za wengi, hupata uungwaji wa wengi kiasi cha kuaminiwa na jamii.
Hawa ni watu maarufu wenye kubeba dhamana ndani ya jamii. Huwa na nguvu ya ushawishi kiasi ya kuwa chachu ya mabadiliko ndani ya jamii husika.
Ndio maana wakati wa shughuli mbalimbali za kijamii kama vile mikutano ya hadhara, kampeni za kisiasa na kijamii, watu maarufu wamekuwa wakitumika.
Watu maarufu huathiri jamii kwa kila wanachokifanya ndani ya jamii. Kutokana na uwezo huo, wanaweza kupandisha ama kushusha thamani ya kitu ama jambo lolote.
Ni kawaida kukuta watu wanabadili mitindo ya maisha kama vyakula, vinywaji, mavazi, mapambo, miondoko na mengine mengi ili kuwa kama mtu fulani maarufu.
MCHANGO WA TEHAMA KATIKA KUKUZA UMAARUFU.
Katika nyakàti hizi za mapinduzi ya teknolojia ya habari na mawasiliano, suala la kuwasiliana na jamii limekuwa jepesi na lenye gharama nafuu.
Mitandao ya kijamii kama Facebook, WhatsApp, telegram, Instagram pamoja na vyombo vya habari yamekuwa majukwaa muhimu kwa watu maarufu kuiathiri jamii.
Makampuni ya mitandao nayo huingiza mapato mengi kutokana na kuwa majukwaa ya kukutanisha watu maarufu na jamii.
WATU MAARUFU NA BIASHARA
Watu maarufu ni zao la jamii ambalo mara nyingi jamii hususani watu wa kawaida huwa hawalitumii ipasavyo. Tunaona mashirika, makampuni binafsi na hata taasisi mbalimbali za serikali wakiwatumia watu hawa katika shughuli zao.
Watu hutazama matangazo ya biashara za makampuni makubwa kupitia watu maarufu ikiwa ni wasanii, wanasiasa, wanamichezo na kuongeza idadi ya wateja.
WATU MAARUFU NA BIDHAA ZA WANYONGE .
Biashara nyingi katika jamii zinazoendelea zinakumbana na changamoto nyingi za kimasoko. Sababu kubwa ni bidhaa ama huduma zao kutofahamika ama kutoaminiwa na walaji au Watumiaji. Hii ni kutokana na uwezo mdogo wa kushawishi wateja. Kukosa maarifa ama mitaji ya kutekeleza mikakati ya uhamasishaji matumizi ya bidhaa za ndani ndio changamoto kubwa kwa wazalishaji wadogo wadogo nchini.
Kama ilivyo kwa makampuni makubwa, huduma na bidhaa za wazalishaji wadogo zinahitaji kutambulishwa kwenye jamii. Lengo ni kuaminisha juu ya ubora na umuhimu wa kutumia bidhaa ama huduma zao.
Kwa kuwa ipo sera ya Ushirikiano kati ya sekta ya Umma na sekta binafsi, basi Jamii Forum kwa kushirikiana na Serikali kupitia wizara ya viwanda na biashara na sekta binafsi, waandae mikutano, warsha na makongamano kwa ajili ya kukutanisha Watu Maarufu na wazalishaji na watoa huduma wadogo wakiwemo wenye mawazo ya ubunifu. Dhumuni kubwa liwe kufahamiana, kufahamishana, kujenga mtazamo wa pamoja, kufunga mikataba na kugawana majukumu ya kazi.
Hali hii itasaidia kuinua si tu uchumi wa wazalishaji wadogo, bali uchumi wa jamii na taifa kwa ujumla.
WATU MAARUFU NA MTIRIRIKO WA ATHARI KWA JAMII.
Watu maarufu ni rasilimali muhimu katika diplomasia na saikolojia ya masoko. Kuanza Kuwatumia katika kutangaza bidhaa za wazalishaji wadogo kutasababisha mtiririko wa athari kwenye mnyororo wa thamani kama vile mauzo na uzalishaji kuongezeka.
Kuongezeka kwa shughuli za uzalishaji na biashara kutasababisha ongezeko la mahitaji ya nguvukazi na wataalamu hususani fani za sayansi, biashara na Sanaa, hivyo kuhamasisha ubunifu na kuongeza matumizi ya teknolojia hali itakayoongeza thamani ya masomo hayo na elimu kwa ujumla.
USHAURI
Wakati sasa umefika kwa wazalishaji wadogo kuanza kutumia fursa za wa watu wetu maarufu kubeba bidhaa na huduma zetu kuyafikia masoko ya ndani na yale ya kimataifa.
Ili kutekeleza hilo mambo kadhaa yanahitaji kuzingatiwa.
Moja, ubora wa bidhaa tunazozizalisha kupitia shirika la ubora Tanzania (TBS) Ili isisababishe kuharibu taswira na haiba za washirika hao mbele za jamii watakayoitangazia bidhaa.
Pili wazalishaji na wabunifu hao wazingatie taratibu za kisheria kama vile usajili wa bidhaa au mawazo ya ubunifu (Hati miliki) kutoka COSOTA au kwa bidhaa kupitia wakala wa usajili wa biashara na makampuni (BRELA) Ili waweze kufanya mikataba ya kibiashara katika kutangaza bidhaa zao.
Tatu ni kwa watu maarufu na ushawishi mkubwa kwa jamii kuwa na mtazamo wa kuwaona wazalishaji wadogo kama washirika wa kibiashara kama walivyo wazalishaji wakubwa.
Nne, mtawanyiko wa shughuli za kiuchumi ndani ya jamii ndio mtaji wa vyanzo rafiki, endelevu na himilivu vya mapato ya serikali. Pamoja na kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati, serikali ihakikishe inaongeza ujazo halali wa fedha kwenye mzunguko sawa na mahitaji ya Karne ya 21 kulingana na idadi halisi ya watu kwa sasa.
Kwa kuwa asilimia kubwa ya fedha kwenye mzunguko hutokana na mishahara, basi serikali iongeze kuajiri watumishi kila mwaka wa fedha kujaza ikama.
Pia serikali iendelee kuboresha mishahara, marupurupu na maslahi ya watumishi wa umma Ili kuruhusu fedha zaidi kuingia kihalali kwenye mzunguko kukidhi shughuli za kiuchumi kuhudumia idadi halisi ya walio nje ya mfumo rasmi wa ajira.
Kwa mfano, kwa mujibu wa takwimu za kiuchumi Tanzania, pato la mtu mmoja mmoja liliongezeka kutoka dola za kimarekani 1,076 kwa mwaka 2020 hadi kufikia dola 1,136 mwaka 2021 sawa na ongezeko la dola 60.
Ongezeko hili lilisababishwa na ukuaji wa shughuli za kiuchumi kwa asilimia 5.49 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia -0.86 mwaka 2020.
Pamoja na sababu nyingine, ukuaji huo wa kiuchumi ulitokana na kuongezeka kwa ujazo wa fedha za bajeti ya matumizi ya kawaida baada ya upandishaji madaraja na ulipaji wa madeni mbalimbali ya watumishi wa umma.
Sambamba na hilo serikali idhibiti upandaji holela wa bei za huduma na bidhaa. Lengo ni kuongeza nguvu ya manunuzi na kuimarisha soko la ndani.
Mwisho, serikali ianzishe mfuko wa kitaifa wa teknolojia. Fedha ikusanywe toka sehemu ya ushuru wa bidhaa zinazoingizwa nchini. Lengo ni kuendeleza teknolojia za ndani na kuongeza matumizi ya sayansi na teknolojia katika shughuli za wazalishaji wadogo wadogo kupitia maeneo maalumu yatakayoanzishwa kwa ajili ya kuchakata na kufungasha bidhaa kufikia viwango vya kimataifa.
Tunataka kutumia uingizaji wa bidhaa nchini kama nyenzo ya
kufikia viwango na masoko ya nchi nyingine na hasa zile zenye uchumi imara.
Lengo ni kujenga na kuimarisha uwiano wenye mizania baina ya nguvu ya wazalishaji na nguvu ya walaji nchini Ili kuwezesha jamii zetu kuishi katika dhana na falsafa ya "kutegemeana kiuchumi" kitaifa na kimataifa.Jamii ni mkusanyiko wa watu wenye hali na mitazamo tofauti wakiwa chini ya mamlaka moja ambapo kila mmoja ana mchango kwa maisha ya mwingine.

Upvote
5