2013
JF-Expert Member
- Aug 2, 2011
- 11,360
- 6,069
wana JF, katika utafiti wangu mdogo, nimeona kuwa kuna watu wanaopendwa sana nje ya familia zao na kuonekana wakarimu, watoa misaada ... mara nyingi hawako hivyo ndani ya familia zao. Japo ni ukweli kuwa hawana ugomvi na mke au watoto lakini mienendo yao mara zote haitazami nyumbani kama inavyotazama shida za watu wasiowahusu.Bahati mbaya watu hawa wanaweza wakawa hata wafanya ibada n.k. lakini haibadilishi hulka yao.mara nyingi familia zao zinaishi kama za watu wasio na uwezo hata kama wao wanauwezo.
Ni watu wasiotoa kipaumbele kwenye kufikiria familia zao kama wafanyavyo kwa mambo ya watu wengine baki. Bila kutaja majina ya watu maarufu ninao waona, pengine katika mitaa ninayoishi hili jambo nimelishuhudia mara kadhaa.Kutokana na hilo inaonyesha upendo kama upendo haugawanyiki, ikiwa utazidisha nje basi kuna uwezekano ukapungua nyumbani.
nadhani watu hawa wanatatizwa na saikolojia ya kupenda kukubalika na jamii.
kwao sifa za nje ni kilakitu kwao wanalewa kuliko hata sifa kwenye familia zao.