Watu maarufu wenye asili ya Afrika na historia ya Afrika

Watu maarufu wenye asili ya Afrika na historia ya Afrika

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
OLAUDAH EQUANO (1745 -1797)
5ce34517e68d2f9648293e3727a9849d.jpg

Ifahamike kuwa katika histori ya Afrika hasa kwa upande wa Afrika magharibi, biashara ya utumwa ilishamili kwa kiasi kikubwa sana. Kulikuwa na idadi kubwa ya Waafrika waliokuwa wakichukuliwa na kupelekwa katika mabara ya Amerika kama wafanyakazi wa mashambani na migodini. Wapo waliochukuliwa wakiwa na umri mdogo na wapo walichukuliwa wakiwa na umri mkubwa.

Hakika historia ya biashara hii ilidumu kwa miaka 400, yaani kuanzia. Biashara hii ilikuwa na matokeo hasi na chanya kwa mabara yote, yaani Afrika, Amerika kaskazini na Amerika kusini. Na mwisho kulizuka watu wa aina mbalimbali walioleta mchango mkubwa sana.

Miongoni mwa watu hao ni Olaudah Equano. Olaudah Equano ni mwafrika aliyezaliwa huko Afrika magharibi nchini Guinea. Alitekwa na wafanyabiashara ya utumwa na kusafirishwa mpaka Amerika kama mtumwa.

Wakati huo, kulikuwa na vita kati ya mwingereza na mfaransa,hivyo Olaudah aliuzwa kwa kiongozi wa meli ya kivita (Royal Navy) na kuhaidiwa zawadi mwisho vita. Kazi aliyokuwa akifanya Olaudah ilikuwa ni kubeba Bunduki (Gunpower), na wakati huo akiwa kwnye meli hiyo ya kivita, alijifunza kusoma na kuandika.

Baada ya vita vile mwingereza alishinda, lakini Olaudah hakupewa chochote, badala yake aliuzwa kwa kapteini mwingine na kumpeleka Olaudah katika visiwa vya karibiani huko Montserrat .

Kutokana na kuwa na uwezo wa kuandika na kusoma, aliweza kuandika kitabu ambacho kilihusu kupinga utumwa ( Ant-Slavery) , kilipata mauzo ya kimataifa kwani kilimuingizia pesa nyingi na kumwezesha kununua uhuru na kufanikiwa kuoa mwanamke wa kizungu aliyeitwa Susanna Cullen mnamo miaka ya 1792.

Japo alifariki miaka 10 Kabla ya Mwingereza Kuanzisha kampeni ya kuzuia biashara ya utmwa mwanzoni mwa miaka ya 1810’, ila kitabu chache kilitoa mchanmgo mkubwa kwa waafrika waliokuwa ndani na nje ya bara la Afrika. Hivyo waaafrika tulikuwa na wasomi hata kabla ya ukoloni kuingia hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom