Rich Hash
Senior Member
- Mar 7, 2017
- 149
- 203
Katika historia ya ulimwengu, hali ya mwafrika imekuwa ikidunishwa mno.
Ni kawaida Afrika kuhusishwa na magonjwa, vita, ujinga au mambo mengine mabaya.
Sio rahisi kuangalia vyombo vya magharibi ukaona mazuri ya Afrika. Utaona tu jinsi wagonjwa wa ukimwi huko Afrika Kusini, Mapinduzi ya Kijeshi, Mauaji na Ukame tu Afrika ya Kati.
Lakini ipo hivi, Katika historia ya Ulimwengu huu, mtu tajiri zaidi kutokea ni mwafrika.
Mansa Musa I ambaye alikuwa mfalme wa himaya ya Mali ndiye mtu tajiri zaidi toka kuumbwa kwa ulimwengu huu.
Alitawala eneo ambalo kwa sasa linatambulika kama Mauritania, Senegal, Gambia, Guinea, Burkina Faso, Niger, Nigeria, Chad,Ghana na Mali yenyewe huko Afrika Magharibi.
Mpaka anafariki mwaka 1331 alikuwa na utajiri unaofikia dola za Marekani bilioni 400(kwa miaka kadhaa mtu tajiri ni Bill Gates mwenye utajiri unaofikia Dola bilioni $85.9)
Mansa Musa I alizaliwa mwaka 1280 na alikuwa kiongozi shupavu kwenye eneo lililozalisha robo tatu ya dhahabu na chumvi yote ulimwenguni kwenye karne ya 14. Haitoshi alijenga Misikiti mingi na kuboresha huduma za kijamii kama elimu na afya.
Alifanya safari ya kuhiji Makka karibu maili 4000 toka Mali, katika msafara wake aligawa dhahabu njia nzima kwa masikini wasiojiweza. Katika msafara wake kulikuwa na ngamia na farasi wapatao 400, Askari na Watumwa. Safari hiyo ya kuhiji inaaminika kuwa iliishitua falme za ulaya na Asia kwani ilikuwa ni ya matumizi makubwa kupata kutokea.
Alitawala Mali kwa miaka 25 na alipofariki mwanae aliyeitwa Maghan I alichukua madaraka.
Wanahistoria wote wanakubaliana karne ya 13 na 14 utajiri wa dunia ulikuwa chini ya himaya ya Afrika hasa magharibi.
Lengo la historia si kukumbusha tu kuhusu zamani bali pia kukueleza tulipotoka. Afrika ilikosea kitu gani karne ya 15 na kuitwa bara la giza?
Imeandikwa na Francis Daudi