Kiwalani finest
Member
- Jul 6, 2024
- 97
- 72
WATU TUNGEKUNJULIANA ROHO, TUKASAIDIANA, TUKAUCHUKIA UNAFIKI, UCHAWA NA UBINAFSI, KUSINGEKUWA NA MATATIZO.
LAKINI ROHO MBAYA NI KIKWAZO.
Nilisikika huko ndotoni nikiwa nakoroma kama simba aliyekamata windo... nikaaza:
"Ni lazima tuseme. Tusiposema, Taifa litaendelea kuhujumiwa."
Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, akiongea na wanahabari tarehe 12/11/2024, alisema:
"Tukiendekeza vitisho, tutadumaza uhuru wa watu kutoa maoni yao, na mwisho wa saa, haina faida yoyote kwa nchi yetu."
(Mwisho wa kunukuu)
Baadhi ya wanasiasa hawasomi Ilani, Katiba, Kanuni, miongozo na taratibu. Hawana hofu ya Mungu, ni ma-actors na ma-actress waliotawaliwa na unafiki, wakitegemea sifa za machawa kusherehesha upotovu wa jamii.
Sheikh Muharram Rashid Mziwanda, katika maulid ya Mtume tarehe 28/11/2024, alisema:
"Msingi alioufundisha Allah Subhanahu Wata'ala kupitia Mtume Muhammad (S.A.W.), ni kwamba binadamu anatakiwa kuishi kwa elimu na akili. Akili pekee ni shida, elimu pekee ni shida."
(Mwisho wa kunukuu)
Viongozi lazima wafungamane na elimu iliyomo kwenye Ilani, Katiba, na miongozo ya kimfumo, huku wakifuata kauli za viongozi wakuu wa kitaifa. Ni ajabu kwamba tunapuuza maandiko na kuyakumbatia machawa.
Askofu Stephano Lameck Musomba, tarehe 03/10/2024, alisema:
"Chawa wanatoka kwenye nguo chafu, sababu ya uchafu wao. Unayejiita chawa unakubali kunywa uchafu wa nguo chafu na uko tayari hata kuasi dini yako."
(Mwisho wa kunukuu)
Laiti tungechukia uchawa, hakuna ambaye angeumia ndani ya nchi tajiri kama hii. Tunapoendelea kuwa wanyonge, machawa wenye roho za ubinafsi wanatulazimisha kuishi katika umaskini na mateso.
Hayati Rais Dkt. John Pombe Magufuli, tarehe 12/07/2016, alisema:
"Ukiona mtumishi wa umma ha-move kwenye direction inayotakiwa, mtoe. Usimlee, aondoke."
(Mwisho wa kunukuu)
Nyakati hizi, uchawa umewatawala watu hadi kuuza mali za Chama bila kufuata kanuni za fedha. Viongozi wachache waovu wameunda himaya zao kwa hila na unafiki, wakilazimisha mambo kwa msaada wa machawa.
Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, tarehe 12/11/2024, alisema:
"Tusichoke kufundishana. Mapungufu yataendelea kupungua."
(Mwisho wa kunukuu)
Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 14/11/2024, akiwa msibani kwa Lawrence Mafuru, alisema:
"Ukiwa hai, fanya kazi, changia hoja na ushauri wenye faida kwa Taifa. Ukiondoka, uondoke ukiwa mtupu."
(Mwisho wa kunukuu)
Nitaendelea kuchangia mawazo ya msingi kwa ajili ya kuinyoosha Taifa, hadi liwe mti ulionyooka na kivuli chake kinyooke pia.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
—Mathias Mugerwa Kahinga