Watu wa Arusha na haraka zao!

Hossam

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2011
Posts
3,544
Reaction score
2,169
Salaam,

Nilipata wasaa wa kutembelea ndugu jijini Arusha takribani wiki mbili zilizopita. Nimejifunza experience mbaya sana ya angalau idadi kubwa ya wakazi wa Arusha bila kujali umri wao.

Watu wana haraka zisizoeleweka na hawana ule ustaarabu wa kusubiriana au kupena muda wakati wa kupewa services kama vile manunuzi ya bidhaa dukani, kwenye migahawa nk.

Bodaboda:
Hawa hawajali foleni, traffic lights, kona mbaya, wala jam. Ni kama wanajeshi wa Taleban. Ukiwa na gari utatakiwa kuwakwepa wewe ama laah watafunga breki kwenye bampa na huna cha kuwafanya. Ukimpa konde zito mmoja utaona tabu ilipo. Hawa wanaamini Ngarenaro ni kubwa kuliko Arusha. Hawa wote simu zao ukimpigia kwanza hamtaelewana mapema halafu ukimeza mate keshakata simu.

Wateja:
Wengi wa wateja hawawezi kupanga foleni. Wana haraka sana. Unaweza kuwa dukani unapewa huduma yeye akaja kwa fujo sana kutaka ahudumiwe haraka. Hali iko hivyo katika foleni benki, sheli nk. Hawa wateja mara zote huwa na hasira sana.

Madereva:
Hakuna fair driving. Huko watu wanapambana nani anakata kona mapema au nani anafika anapokwenda mapema. Ukijichanganya uingie barabarani wanakata pua.

Watembea kwa miguu:
Hawa hawana tofauti sana na ndugu zao wa Bodaboda. Hawa wao kukatisha barabara hata pasipo na zebra ni kawaida sana. Tambua mapema kuwa kwenye mataa green light siyo lazima wao wakusubiri. Utalazimika kuwasubiri wao na Ole wako mguse mmoja.

Ni mimi Pangu Pakavu.
 
Arusha ni republic kamili ukifika lazima uanzishe uzi maana ni ndoto ya wa Tz wengi
Haya tuambie ni mkoa gani Tz Bodaboda ni wastaarabu?
Fujo unazo zisema zipo barabarani hazina ukweli wowote kama kweli zingekuwepo basi kila siku zingeripotiwa ajali mbaya
 
Mount Meru Hospital vijana wa Boda wana ward yao maalum. Kila siku wanne lazima wareport!
 
Wapo pia vijana wanaopush Subaru zile zenye makelele sana. Aisee hawa ukimuovertake anakukimbiza bila kujali unaelekea wapi. Hawa nao huwa hawapendi kupitwa hata iweje. Utamuona anakakamaa anakanyaga mafuta hata kama ulikuwa unaelekea Ngaramtoni yeye kwa hasira alizokuwa nazo anasepa hadi Namanga!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…