Watu wa Hip-Hop ebu tukutane hapa kidogo

Watu wa Hip-Hop ebu tukutane hapa kidogo

barcelonista

Senior Member
Joined
Apr 26, 2021
Posts
158
Reaction score
149
Wakuu kwema?

Watu wa Hip-Hop ebu tukutane hapa kidogo,,,Hivi ni versi gani kali ya Hip-Hop hapa Bongo uliwahi kuisikia mpaka ukasema yes hii ni versi bora kabisa kuwahi kuisikia hadi leo huchoki kuisikiliza,,,

Kwangu mm versi yangu bora ya muda wote alifanya Albert Mangwea kwenye ngoma inaitwa Msela,,,Aliwatesa sana Juma Nature na KR. Bonge la ngoma beat moja hatari mno...

Ngwea aliflow sana,akaitesa sana beat alichana kuhusu life huko mitaani,haso n.k

Nimekuwekea hapa chini hiyo Versi na Audio yenyewe,,,Nambie ww mdau Versi gani ya Hip hop hadi leo huichoki.

R.i.p CowBama....

Yo! Uh
Watu tumeshadata na hili ghetto Life style
Shati back (?) na u-Nelly wa X-Plastaz (What?)
Hey' Dark Master ntembezee chata
Kisha nipe kipaza nihubiri kama pastor
Ndani ya ghetto ni mengi yashatukuta
Lakini' masela bado tunakomaa kutafuta
Bado tunazisaka' hata kwenye vichaka
Mtafutaji hachoki, akichoka ndo ameshapata
Japo sometimes kile kitu unachopata, Ni'
Tofauti kabisa na kile hasa unachotaka
Ila' Mwanaume lazima tu ujifunze kuridhika
Kwani ukichagua sana hukawii kutoka kapa
Duniani wote hatuwezi kuwa sawa
Na ndo maana wapinzani wa jadi mnapagawa (Yeah)
Kama nipo juu 'Ni juu (Uh-Huh)
Ningoje chini, au nifate juu uvunjike guu
Ma Supastaa tuna ng'aa kwa pamba tunazo vaa
Zinaficha njaa

Ila tunapo kaa wengine nyumba ya udongo' nyasi
Mlango wa gunia (Uh-Huh)
Ndani hakuna kikombe, mwiko wala sufuria
Zaidi ya kiberiti tu na kipande cha mkeka
Na nikisha kula (..Ishh! ) 'mambo yangu naya weka
Wala sioni hatari kula Dona Dagaa
Siku nyingine hawa Jogoo nao wanalala na njaa
Na usione tumepinda 'Migongo
Ukadhani' ni vibiongo

Pengine ni ufupi tu wa mlango
We endelea kula bia, Acha mi nkapate Gongo
Ili mradi wote tuwe stimu' ndio life ya kibongo ( Msela!
 
Weka verse basi

Verse ya 2

Deep in my thoughts tryna thinking bout this life
Na bongo bila ya mchongo ujue ni tight
I wanna make it right thats why I don't sleep at night
Hata ikiwa back to back everyday its alright
Its alright kwangu naona poa tuu mazee
Siwazi ka nachoka maana bado niko tee
Sometimes I hear voices in my head
Zingine zikinikiniumiza ilimradi nipotee goddamn
Hujiulizi why napenda tuu kusizi
To me its like a thrill sio kupenga ningekuwa chizi
Vitu vingine niliamua to take easy
Streess ikizidi naenda ufukweni to catch a breez
Utani wa nini kwenye kazi za watu
Kama kweli unajiamini usiwe muumini wa wafu
Ungana na mm ukiamini ka muumini wa mashafu
Siku nnikitusua hapatakuwa na nguvu ya watu
Jitihada zinakuwa zaidi ya mtoto anae tambaa
Asante mungu nmekuwa ingawa baba alinkataa
Siku mtupa nilimjua japo ndugu walishangaa
Ebhanae daah nasonga na sijakata hata tamaa
 
Nakubali wimbo wa CNN-Ngwear ft Fid Q natamani kuona verse ya kwanza sema mistari ya Fid Q migumu msaada kwa anayeweza ashushe [emoji120]hapaa
 
Daah verse ni nyingi sana na zote zinabamba kulingana na mood ambayo niko nayo siku hiyo

Kwenye mood ya huzuni hususani msiba wapo wasanii kibao wenye ngoma kali za kufariji lakini kwa haraka haraka naweza nikachagua mistari kadhaa ya nala mzalendo

Hii taarifa ya ghafla man, tumepatwa na msiba usiulize kafa nani.../

Kama noma na iwe noma kaka mani, fanyeni fasta muibuke maskani.../

Tukae tujadili makamanda, mwenzetu tumsitiri inahitajika sanda.../

Sijui anahisi nini, joto au baridi ila tayari nimemtoa nguo za mwilini.../

Dakika zinakata, na uhakika mmenipata... Nikikata simu mtakua mmeshafika hapa.../

Wapitie makanta waambie tuna uzuni, wampigie mfalanyongo autangazie utamaduni.../

Hatushindwi wanangu hata kama hatuna fedha, hatuwezi kushindwa hata kununua jeneza.../

Hili letu sote limetukuta wana, undugu ni kufa na kuzikana.../
 
Daah verse ni nyingi sana na zote zinabamba kulingana na mood ambayo niko nayo siku hiyo

Kwenye mood ya huzuni hususani msiba wapo wasanii kibao wenye ngoma kali za kufariji lakini kwa haraka haraka naweza nikachagua mistari kadhaa ya nala mzalendo

Hii taarifa ya ghafla man, tumepatwa na msiba usiulize kafa nani.../

Kama noma na iwe noma kaka mani, fanyeni fasta muibuke maskani.../

Tukae tujadili makamanda, mwenzetu tumsitiri inahitajika sanda.../

Sijui anahisi nini, joto au baridi ila tayari nimemtoa nguo za mwilini.../

Dakika zinakata, na uhakika mmenipata... Nikikata simu mtakua mmeshafika hapa.../

Wapitie makanta waambie tuna uzuni, wampigie mfalanyongo autangazie utamaduni.../

Hatushindwi wanangu hata kama hatuna fedha, hatuwezi kushindwa hata kununua jeneza.../

Hili letu sote limetukuta wana, undugu ni kufa na kuzikana.../
Nani huyu?
 
Zipo verse za vituko ambazo ukisikiza tu unacheka

Mfano verse za songa

Kuna kima alinidisi kwa akili ya kukodi, akajua nitampa kiki niki respond.../

Niko fake niko real mi ni pig ya emoji, sa namcheki tu ka gwajima akijirekodi.../

******************************
Haiuziwi kwa under 18 muda usije kumponza mtoto, kama una dozi kunywa hata soda ndogo.../

Mdogo mdogo sio kreti libaki empty, utajikuta bwana mdogo umelost imebaki chenchi.../

Ukaleta tu madrama, afu kutapika ni upimbi.../
Tulisema tule nyama, we ukapiga magimbi.../

Ukalainisha na mtindi, ukadai haipiti kooni sa ukitaka kuleta ugomvi utachapika kwa mlinzi.../

Pombe nzuri huwenda na magoma kwenye hewa, warembo wakali pia nyama choma ka ngekewa.../

Ka ulikuja ukaona kawaida sa unaona kila waiter mzuri nenda home ushalewa.../

Watu wana have fun yani mpaka kuna kucha, wengine washalewa wanaita mama nakufa.../
 
Hisia Ya Nikki mbishi, Part ya Suma mnazaleth.

nnachokumbuka alimuamini kama mchungaji wa kanisa
yote yanayosemwa mitaani hakujua kama yanamgusa
akaona bora afeli shule, mwisho akafaulu mapenzi
mashauzi ndo vile, mwishoni yamekuwa majonzi
hakujua yesu wa mapenzi mitaani watu wangemuita
aliyemuamini kama mpenzi kawa yuda leo yamemkuta
drop love kwenye usasa, so long ka bi kidude
unampenda kisha unamuacha, asikutapeli kama dude
leo anataka second chance ka Salvador Cerrinza
alishachezea first chance ka movie cheki anakonda
rahisi sana kukubali kile ambacho yeye anajua
hata kama atakuja feli kwa vitendo sio kuongea
anakumbuka game tough yeye na mpenzi walizocheza
leo ana'drop kama clove, uchaguzi daily wanammeza
kila anayesoma likizo sio kweli kwamba ana supp
watoto wanawapita kiuwezo watu wazima mpaka wana'STOP!
AH, we utaona unapendwa kumbe ndo unachunwa
we unaona unapanda kumbe ndo unavunwa
ushambandika kama sticker ukimbandua ndo unasepa
usije ukatekeka akakumwaga ka ana tipa
ah, nilipendwa mpaka wapangaji nyumbani wakawa wananuna
leo love imegeuka mtaji kwenye mzani watu wanapima
sio siri haya mambo nimeshayaona kijana
demu fulani kamteka mwana mpaka mia anabana
washatumia sana pesa kisha wakaja achana
demu kahongwa mpaka chaser kumbe kuna boya anambana
sio kila anayebeba begi ukadhani shule anaelewa
 
Back
Top Bottom