Watu wa kawaida sana ila ndoa zao zimedumu muda mrefu sababu ni umaskini au mapenzi ya dhati?

Watu wa kawaida sana ila ndoa zao zimedumu muda mrefu sababu ni umaskini au mapenzi ya dhati?

kadogo2

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
1,889
Reaction score
3,059
Nimejiuliza sana mpk nikawauliza why wamedumu muda mrefu wakati kuna wenzao ndoa zao zipo chali…

Ninapokaa nipo kwa wazazi, mtaani tumezungukwa na wazaramo wengi na wagogo

Kuna majirani zetu ambao ni Kama familia sasa tumewakuta na wao ndio walisimamia mpk ujenzi wa nyumba yetu kukamilika hivyo walitupokea… sasa huyu jirani yetu ana watoto wakike na kiume, wenginee ni wa kuwazaa mwenyewe wenginee ni watoto wa ndugu zake ambao wamelelewa hapo mpk kujitegemea

Mtoto wake wa kwanza alipomaliza 4m4 akahozeshwa na mwanaume ambae alikuwa jirani yetu ila bi dada hakuwa hakimpenda huyo kaka wakaachana ndoa ikiwa na wiki mbili bibie akidai jamaa jogoo hapandi mtungi,, hakuchukua hata muda akaoana na mwanaume aliekuwa akimtaka yeye mpk leo wapo mtoto wao wa kwanza yupo darasa la 5 miaka 10 ina maana ndoa yao ina miaka 11… na hapo walioana wadogowadogo yaani bi dada anaweza kuwa wa 94 na huyo kijana havuki 92

Mtoto wa pili nae alioana na kijana mmoja hawakulast wakaachana, huyu aliozeshwa alipovunja ungo akiwa anatolewa mwali siku ile ile na ndoa juu.. alibahatika kuzaa na huyo kijana mtoto mmoja. Ameshaolewaga na mtu mwingine ambae yeye alikuwa anamtaka mtoto wao wa kwanza yupo na miaka 9 na ndoa yao ina miaka 9

Wa tatu nae ndoa yake ina Miaka 10 yeye ameolewa na huyohuyo mpk Leo

Sasa ni nini sababu ya hao watu kudumu sana kwenye ndoa ni sababu ya umaskini au wanawake kuwapenda wanaume kuliko wanaume zao wanavyowapenda

Kinachonishangaza hawa watu wameona wakiwa watoto sana imagine binti ana miaka14 kijana Miaka 18 ila mpk Leo wapo pamoja wanadunda na wameoana ndoa za kiislam kabisa
 
jibu hapo ni Upendo wa kweli.

Ndani ya upendo kuna mambo yote ya muhimu yanayosababisha ndoa kuendelea kuwa na uhai.

Upendo wa kweli hutii, hueshimu, hujali, huvumilia, hulinda, husamehe, husikiliza na mengine mengi yenye kujenga afya ya wapendanao.
 
Huenda nikawa sijui. Nini maana ya ndoa kudumu mkuu?

Ni muda Gani huvhukulia kuwa hii ndoa imedumu?

Unajua ndoa sasa hivi kutoboa 3 years ni ngumu haswa hizi ndoa za vijana ndio maana nimeshangaa hao vijana mpk Leo wapo na still ni younger
 
Ukiangalia kwa umakini sana izo ndoa hapo hakuna influence wala matarajio ya mali/ pesa/ uchumi.

Nafikiri ndio sababu ya ndoa zao kudumu.

Sasa sisi unao uishajipata vizuri sana kumbe mwenzako kafuata unafuuu wa maisha na uchumi tu.
 
Ukitaka udumu kwenye ndoa na mahusiano yakawa bora ni hizi sifa .
Heshima
Kuwa na mipaka na sehemu katika ndoa
Kusikilizana
Kujaliana
Nakuwa muaminifu na mkweli
Kusamehe nakutokuwa na visasi na vinyongo kutopenda sehemu isiyoyahusika ambayo mola alikataa kutumika .
Kutonyanyasana nakutaka kupanda watu kichwani.
Kutambua uwepo wa mwenzako na atambue wako.
Kuepuka ugomvi usio nakichwa wala miguu kuwa na wivu wakiasi .
Kuwa na ubunifu katika mapenzi na kufurahia tendo la mwenzako.
kumuona mtu wako anadhamani hadi siku yakufa kwako. Kushukuru kwa kidofo hadi mpate kikubwa ukiwa hivi . Mtadumu .
 
Ukiangalia kwa umakini sana izo ndoa hapo hakuna influence wala matarajio ya mali/ pesa/ uchumi.

Nafikiri ndio sababu ya ndoa zao kudumu.

Sasa sisi unao uishajipata vizuri sana kumbe mwenzako kafuata unafuuu wa maisha na uchumi tu.

Hii inaweza kuwa kweli
 
Back
Top Bottom