Kwanini muwaibie watu wanaotafuta vyao vya halali Kwa jasho na damu? Utanijibu kwanini watembeze kichapo mtaa mzima ilihali sio wote walioshiriki kumuibia?Uku mtaani Kuna mtu wa mamla ameibiwa, Sasa kimetembezwa kichapo Jana.
Mmh kwa wajuzi mnaojua Mambo hao Jamaa wakiibiwa ndo mwendo wa kutudunda makabwela,
Au Ndio washika mpini na mshika makali.
Duuu Duniani Kuna shida Kinoma.
Daaa Kuna Watu wanaishi kwa Raha Ila sisi wengine tunasindikiza wanaoishi.
Kwa kichapo nilichokiona mtu akichwapwa.
"Usiamini ktk sheria, wapo watu wapo Juu ya sheria na wanaweza kufanya watakalo popote na mda wowote"
Kwanini muwaibie watu wanaotafuta vyao vya halali Kwa jasho na damu? Utanijibu kwanini watembeze kichapo mtaa mzima ilihali sio wote walioshiriki kumuibia?
Jibu ni kwamba, mtaa unaoshiriki kuwaficha wahalifu nao ni sehemu ya uhalifu kwahiyo wanapaswa kulipia gharama pia.
Siungi mkono vitendo vya kujichukulia Sheria mkononi, Ila ni vyema jamii ikaacha kufumbia macho uhalifu na wahalifu Kwa kutoa taarifa Kwa mamlaka husika kwaajili ya kuchukua hatua stahiki.