TheDreamer Thebeliever
JF-Expert Member
- Feb 26, 2018
- 2,490
- 3,584
Habari wana JF,
Natumai wengine mshalala usiku huu, ila kuna jambo mkiamka nitaomba tulijadili sababu ni miezi kama sita sasa "Mamsap" wangu alikuwa anataka feedback ya biashara ya kusafirisha madumu ya mafuta na magunia tupu.
Kifupi alikuwa anataka niwe namtumia madumu ya mafuta na viroba vya unga (empty) ili ayauze kama vibebeo au vifungashio kwa wakulima huko Kyela- Mbeya baada ya kuvuna mazao.
Binafsi sikumuelewa vizuri nikajua ni mtego wa upigaji maana "mababy mamas" ndiyo michezo yao, hivyo ilinichukua miezi takribani sita bila kumpa mrejesho.
Wiki iliyopita nilipita na gari yangu katikati ya jiji la Dar mitaa fulani K/koo nikaona rundo la madumu yalisiyo na mafuta yamekusanywa kitaa fulani hapo ndipo kichwa kikaanza ku-click mamsap alichoniuliza.
Basi ikabidi ni-park pembeni kwenda kutafuta taarifa maeneo yale. Kama unavyojua Wabongo wanaweza kukupa siri za ndani za wake zao yaani unaweza kukutana na Mbongo hata hakujui anaanza kukupa mastori ya town mara hoo wife jana kaninyima unyumba, mara ooh yaani utapewa kila umbea ila sio siri za biashara (kifupi nilitoka kapa).
Hapo ndipo nilipoamua kufanya ujasusi wa kibiashara. Kesho yake nilirudi nikiwa na kibukta changu (very simple) chini kandambili papa na nguru na katisheti kangu nikajichanganya kwenye kijiwe cha alkasus nikakaa kama masaa mawili kukusanya taarifa. Baadaye nikaenda kuzungumza na wale madogo wanaofunga mzigo.
Kifupi nilibahatika kupata taarifa (information) za kutosha kuhusu upatikanaji (supply side), ila kuhusu taarifa za uhitaji (demand) sikufanikiwa.
Kwa wale mnaotoka mikoa kama Kigoma, Mbeya, Singida n.k ningeomba mshee nasi uzoefu wenu kuhusu:
1) uitaji wa madumu, mifuko ya viroba vya unga, visado n.k upo vipi huko.
2) Naomba kujua bei za kuuza kwa huko kama nikija na mzigo wangu.
3) Miezi gani ina uhitaji mkubwa (Higher demand)
Asanteni wadau, naomba kuwasilisha na nikaribishe wachangiaji kutoka pande zote.