Hivi kwenye jambo lolote linalohitaji kibali cha Rais, au waziri wa sector husika, kunapotokea kuna mkataba kama ule wa DP WORLD, Rais au waziri anapitia kwanza au kuna watu wanapitia kwa niaba yake halafu baadaye yeye anaonyeshwa tu pa kuweka sahihi?
Na kama ikatokea kuna mikataba ya nchi na nchi, TISS, police, jeshi wanhusishwa kweli? hivi ni vyombo vya ulinzi na bila shaka ushauri wao kwenye maeneo nyeti ni muhimu.
Na je kama Rais amefanya kinyume na matarajio ya nchi, nani anamwambia hapana au ndio. nauliza hivyo kwa sababu kama bunge letu lenye mawaziri na wasomi wa kila aina wamesema Rais yupo sahihi nani tena wa kumkosoa?
Makatibu wakuu wa sector wanahusishwa kuhusu mikataba hii?