Watu wa wizara ya afya ni kweli mmefundisha mambo haya?

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Iko hivi, kuna mgonjwa aliandikiwa artesunate inj, lakini ilikosekana na badala yake akapata artemether inj. Nesi alikataa kumchoma eti hiki ni kitu kingine kabisa na walifundishwa na wizara ya afya wachome artesunate tu.

Na akaendelea kusisitiza eti ni bora achome Quinine kuliko hiyo artemether. Sasa nauliza kimsingi, kuna tofauti gani ya dawa hizo mbili?

Inayopigiwa debe imetengeneza China, na inayokataliwa imetengenezwa Belgium. Zote ni kutoka mmea unaojulikana kama artemesia alua (mtanisahihisha).

Je kama ni kweli mmezuia wasichome artemether, hii si matokeo ya milungula inayotolewa na makampuni ya kichina ili wauze dawa zao?

Na kama artemether inj ina matatizo kwanini TFDA haiindoi sokoni?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
hizo dawa ziko kundi moja la artemisinin ila ni dawa tofauti mbili.kwa mawazo yako unataka kusema ni dawa moja ila majina na manufacturing tofauti. tofauti ya hizo dawa ,artemether ni lipid solube na artisunate ni water soluble, half life ya artisunate ni 45 min na artemether ni 4-11hours . efficase zote zinalingana zidi ya malaria kali. lakini kwa tanzania guideline inasema chaguo lakwanza kutibu malaria kali iliyoshindwa na dawa zingine ni injartesunate
 

Moja acha ujivuni na pili toa maelezo kwa kina.
 

Sina tatizo na lipid au hydro solubilities,pia sina tatizo na tofauti hizo kimsingi,shida yangu NI "kweli kwamba ukikosa artesunate inj,artemether ni kitu kingine kabisa ambacho hakiwezi kuwa mbadala na badala yake ni bora itumike quinine?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…