"Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

Shein amesema huu siyo wakati wa kujadili articles za Muungano, ni vita ya corona. Wewe mwandishi mtegemewa na jamii kuisemea unaleta habari isiyokuwa na maana kipindi hiki watu wanapukutika. Leta "nondo" hapa tuone tunafanyaje!


Bahati mbaya sana pana agenda za wazi za kudunisha suala la Corona inavyoonekana kwa gharama yoyote.

Angalia TV hata radio zetu.

Compare coverage ya Corona Tanzania katika vyombo hivyo na coverage ya Corona nje ya nchi.

Utadhani sisi Corona haituhusu.

Tunachapa kazi. Tunajadiri kero za muungano na hata vijiti vya 2020 na 2025.

Tuna vitu haiko sawa!
 
Mwanamke ambaye naweza kumpigia kura kwa Tz ni kati ya hawa wawili: 1 Fatuma Karume na Maria Sarungi, hawa ni watoto wa viongozi wakubwa sn hapa TZ lakini wamekataa kuwa sehemu ya mfumo ambao keki ya Taifa wanakula wachache, hawa wadada kaka zao wameshindwa lakini wenyewe wameweza wanapigania maslahi ya nchi na siyo maslahi yao binafsi, Fatuma Karume na Maria Sarungi kama siyo kupigia maslahi mapana ya Wtz sasahivi wangekuwa mawaziri.
 
SAMIA kajazwa "roho mtakatifu" na anampenda YEsu!
Huyu mama hata kama ni mama yako, the way anaongea aisee, so sweeet and humble, eeh Mungu mpe mama huyu miaka aone wenzake ma dikteta wakiangamia.


Hahhhaahhahahhaahhaa nimelia baada ya kucheka jaman🤣🤣🤣🤣🤣! Dah..sijui umewqza nini jamni..tuhurumieni mbavu jaman
 
Anazungumza vizuri kwa unyenyekevu mpaka raha.[emoji15][emoji15][emoji15]

Kwahiyo unaibiwa kirahsi vile kwa maneno matamu hata kama ni ya kilaghai.?

Sijasoma bandiko lote, nimeishia hapo tu... acha niimagine hiyo mpaka raha.[emoji39]
 

Usiwe mjinga, wapo upande wa pili kwa kazi maalumu... mojawapo ni hiyo kukufariji wewe ujione mwenzao.
 
Kaka Pascal Tabia ya mtu huwezi kuipima kwa mazungumzo pekee yake. Suala la kuwa vizuri katka kupangilia hoja ya mambo ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania sio credit za kujiridhisha Kama mtu huyo atauweza urais ipasavyo.

Kwa mitazamo yako kwa kigezo Cha logic katka kufanya analysis ya mambo ndio sifa kuu ya kuwa kiongozi mkuu wa nchi Basi Leo hii tusingekuwa na Rais Kama Dr John P. Magufuli pamoja na sifa kedekede ambazo umempa Mara nyingi kuhusu utendaji wake katika Taifa Hili.
Pascal utakubaliana na Mimi kwamba Rais Magufuli hayupo vizuri Sana katka kupangilia hoja lkn yupo vizuri katka kusimamia kile anachokiamini na baadae kuleta mawazo chanya kwa wananchi. Usipokubaliana na Mimi Basi wewe Ni msifiaji tu bila kujua unachosifia kina nantiki gani ukirejerea post zako nyingi zipo humu za kusifia utendaji mzuri wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania . Na ukikubaliana na Mimi kuwa uongeaji sio utendaji Basi post yako hapa juu haina mantiki yoyote zaidi ya kusifia facial expression ya Mama Samia

Kwahyo mi bado nakupinga kwamba upangaji wa hoja sio kigezo Cha kuwa Rais. Tanzania Sasa hatuhitaji viongozi wa kusimama majukwaani wakipanga hoja kwa umahiri ya mikakati lakn utendaji mbovu. Tunahitaji kiongozi Mwenye Kutenda zaidi kwa wananchi sio porojo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal Mayalla,
Visiwani wanasiasa hawafanyi "doublespeak" Tell It Like It Isn't: A Campaign Guide to Political Doubletalk . Kweli labda yupo CCM ila moyo upo upinzani. Na historia ya kisiasa Zanzibar lolote linaweza kutokea maana tunaona huko Zanzibar jaji mkuu Ali Haji Pandu kujiuzulu, Maalim Seif waziri kiongozi kujiuzulu, makamu wa kwanza serikali ya maridhiano SMZ kujiuzulu Seif Sharrif Hamad, mwanasheria mkuu wa SMZ kujiuzulu .....listi ni ndefu vigogo waZanzibari halafu wanajitoa au kufukuzwa CCM na kujiunga kambi ya pili yaani almaaruf upinzani.

February 17, 2020

FULL HISTORIA YA MAMA SAMIA

Mama Samia anakubali hoja nzito za wapinzani, nilikataa pendekezo la kuwa Makamu wa Rais

Makamu wa Rais wa serikali ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Hassan Suluhu asema kilichomsukuma kuingia katika siasa ni maoni na hoja za mashiko za wapinzani Bungeni / Baraza la Wawakilishi ambazo hazijibiwi vyema kwa hoja na mawaziri wa serikali.

Hilo la kukerwa na majibu ya serikali yasiyokidhi hoja za wapinzani, Mama Samia akajiona ni kama Activist / Mwanaharakati ingawa ni CCM anayehusudu maswali magumu yajibiwe kwa hoja thabiti.

Mama Samia anaongeza kabla ya kuingia siasa alikuwa anaona nondo za wapinzani huku upande wa serikali ambayo ni ya CCM bara na Visiwani pia, mawaziri huja na majibu hafifu yasiyo ridhisha kwake na wanaofuatilia shughuli za Bunge.


Pamoja na kukunwa na hoja zilizoenda shule za wapinzani, Mama Samia aliwaeleza wasikilizaji ametokea ktk familia ya kawaida ambapo baba yake alikuwa mwalimu wa shule na mama yake mama wa nyumbani aliyetumia nafasi kuwafundisha na kuwasaidia kazi za masomo wakitoka shule.

Hiyo ilimsukuma kujiendeleza kimasomo kila wakati na kufanya kazi katika serikali ya SMZ na muda mrefu katika NGO's mbalimbali za kimataifa kabla ya kujiunga na siasa kupitia viti maalum CCM.

Mama Samia alipofanikiwa kuteuliwa Mwakilishi wa Viti Maalum alipata faraja kubwa akitegemea kutasaidia kukijenga chama cha CCM kuwa na watendaji wajibu-hoja-wazuri, kutokana na kuona mawaziri wa serikali na wabunge wa CCM kukosa hoja motomoto au majibu yakuridhisha kwa maswali na hoja nzuri za wapinzani na kuzidiwa wakiwa bungeni au baraza la wakilishi wakionekana / kusikika 'live' .

Ghafla bin vu, Mama Samia alipoingia Baraza la Wakilishi akateuliwa kuwa Waziri wa Sera Ajira Maendeleo ya akina Mama na Vijana ktk Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Na miaka 5 baadaye akawa waziri wa Biashara na Utalii katika SMZ. Baadaye akagombea kiti Makunduchi Zanzibar na kufanikiwa kuwa mbunge wa Zanzibar katika Bunge la Jamhuri ya Muungano na kuteuliwa kuwa Waziri wa Mazingira na hatimaye mgombea Mwenza wa Urais na kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania.

Hakutegemea kupewa nafasi hizo ghafla hivyo na pia akikumbuka nondo za wapinzani bungeni kupitia maswali, akaona amewekwa mstari wa mbele kukabiliana na hoja zinazowagusa wananchi ambazo hazipatiwi majibu ya kuwaridhisha wananchi.

Source: Millard Ayo

Toka katika maktaba :


Advertisement

Karume, Maalim Seif wakutana faragha Z’bar
Saturday May 3 2014
>Rais Mstaafu wa Zanzibar awamu ya sita, Dk Amani Abeid Karume amekutana na viongozi wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar na kujadiliana hali ya kisiasa iliyojitokeza katika mjadala wa Katiba Mpya, pamoja na kujitoa kwa wabunge wa Ukawa kwenye vikao vya Bunge Maalumu la Katiba.


Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume na Makamu wa Kwanza wa Rais wa SMZ, Maalim Seif Sharif Hamad wakifurahia jambo wakati wa mazungumzo yao nyumbani kwa Karume, Mbweni mjini Zanzibar. Na Mpigapicha Wetu
 
Mama Samia yuko vizuri sana. Tafuta clip alipomtembelea Tundu Lissu pale Hospitalini Nairobi. Utamfaidi Samia orijino yaani bila zile mbwembwe za kisiasa. Mama mmoja mtamu saaana.
 
Binafsi huyo mama huwa ananivutia sana anapozungumza,ana lafudhi tamu ya kiswahili hata na kiingereza pia. Kwangu huo ndiyo ungekuwa mtego wangu kama macho yake yalivyomvutia P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…