"Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

Kweli wewe ni Pascal njaa, unanjaa kwelkwel
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hali ya covid 19 ilivyo katika taifa letu ni vigumu kutabiri nani atakuwa rais wa nchi mwishoni mwa mwaka huu wakuu wanamchezea mgeni sebuleni na hajali idadi ya walinzi wanaomzunguka mzee you never know Pasco imagine wale wazee wa kucheza na kura wakati wako busy kuiba mara paap anaanguka mmojawapo kwa kushindwa kupumua
 
Hii hoja ya uvamizi wa Zanzibar, kisha iwe rahisi kuivamia Bara ni ya kipumbavu kabisa. Inatumika kutishia watu tu.

Zanzibar hata ikiwa haina uhusiano wowote ule na Bara itabaki kama hichi jirani tunayopakana nayo tukitenganishwa na maji.

Sawa ambavyo tunapakana na nchi nyingine tu,Kenya,Uganda,Mozambique,Malawi, sasa iweje nongwa kwa zanzibar eti ni rahisi kuvamiwa.

Kwa sasa hiyo ni hoja. JWTZ wapo imara na vyombo vingine,hata Tanga ikiwa nchi nyingine bado tupo salama.

Sent using iphone pro max
 
Mama Samia yuko vizuri sana. Tafuta clip alipomtembelea Tundu Lissu pale Hospitalini Nairobi. Utamfaidi Samia orijino yaani bila zile mbwembwe za kisiasa. Mama mmoja mtamu saaana.

..mimi namkumbuka Mama Samia wa bunge maalum la katiba?

..Mama akitutana na wana-ccm wenzake hugeuka kuwa mhafidhina.

..Na kiburi na uhafidhina wa ccm unawezeshwa na madaraka makubwa aliyonayo Raisi[mwenyekiti wa ccm] na wingi wa wabunge wao bungeni.
 
utumbo mtupu ni njaa tu inasumbuwa na njaa ndio tatizo la tanzania
 
hakuna janga kubwa duniani kama Uccm bora corona kuliko uCCM
 
Ni kweli mkuu, lakini inaonekana Samia orijino ni mwanaharakati, kama alivyoeleza. Pia ni maverick. Hii ina maana ni kweli mara kadhaa atakuwa alitofautiana saaana na Magufuli. Hebu imagine, Magufuli na ubabe wake kuwaita "Pumbavu" waziri Daktari Mpango na Prof. Kabudi, wanaume, hivi atakuwa kamuitaje Samia, mwanamke? Na Samia naye atachukuliaje?

Pia inaonekana ni mpenda haki. Aliwahi kuwasifia hadharani wabunge wa upinzani bara, kuwa wanajenga hoja vizuri na hata akathubutu kudai wabunge wa ccm wapewe semina! Nadhani system haikufurahia hali hiyo. Na hapa tumemsikia akiwasifia wapinzani katika baraza la wawakilishi kwamba wanajenga hoja vizuri kuliko wa ccm! Na pia kwamba mawaziri wa serikali ya ccm ni waongo. Mtu wa aina hii si anapata taabu sana katika serikali iliyojaa unafiki, ya awamu ya 5?
 
Kwa hiyo mnakubali kuwa, bila kuungana na zanzibar leo hatutakuwa na usalama?
Zenj ikichomoka toka muungano wanajeshi ngangari na jiwe wa Bara wataondoka zenj na Bahari yetu kule itakuwa huru kwa Maharamia wote wa Dunia wa Baharini hasa from Somalia watapiga wazenj tani yao na baharini zenj patachafuka meli zitakuwa zikiporwa na watu kuuwawa na muda si muda Zenj itatwaliwa kwa mabavu na Oman wanaoamini hadi leo kuwa Zenj ni ardhi yao, Zenj itatawaliwa tena na kina Jamshid na Seyyid Said na Barghashi wa kileo ambao wataungana na Qatar na Yemen na Saudia kuishambulia Zenj na kuwakalisha chini wazenj wote kisha Waarab watahamia bongo na kuishambulia bongo na majirani zetu kwa mizinga ya kifaransa ya masafa marefu wanayonunua waarabu kwa sifa siku hizi na sote hatutaweza kushika cm na kuandika hapa JF manake tutakuwa mbio mbio kutokomea Congo DRC na Burundi hadi tutaingia Atlantiki Ocean, tutavuka na kuingia Obamaland!

Kwanza wasumbufu wa muungano wanapoteza focus ya Corona fight sababu walioanzisha Muungano hawapo labda wafufuliwe waje waondoe muungano wao!

Asietaka muungano ahame nchi
 
hidden policies apply!! yaani ni Men and men and men yani Afrika bado sana kwa kinamama!!
kweli ni ngumu kwa africa ila inawezekana tu.helen johnson selif kama vile alifungua mlango.

kwa hapa bongo tushapata spika mwanamke,
makamo wa rais mwanamke.

mwanamke keshafika mpaka tano bora kwenye nomination ya kinyang'anyiro cha urais ndani ya msitu wa ma big fish kama lowasa,membe na wengine,ikabaki chupuchupu kuibuka kidedea,Asha Rose.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makamo au Makamu?
 
Ikipendeza 2020 July achukue form na CC wampitishe kama mgombea.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…